ASUS recommends Windows 10 Pro for business.

  ASUS VivoBook Flip 14 TP410UA

  Rudi juu
  Tija Kubwa.
  Taswira pana.
  ASUS VivoBook Flip 14 ni kompyuta pakato ya kwanza inayoweza kubadilishwa yenye inchi 14 iliyo na ASUS NanoEdge bezel nyembamba sana, inayoruhusu kioo cha inchi 14 cha HD Kamili kukaa ndani ya fremu ambayo ina ukubwa wa inchi 13 sawa na kompyuta pakato ya kawaida.
  VivoBook Flip 14 ambayo ni nyembamba na nyepesi imeundwa kukidhi tukio lolote. Itumie kama kompyuta pakato maridadi, tableti inayobebeka kirahisi — au kitu chochote kati ya hivyo. Processor yake ya Intel® Core ™ i7 inakuwezesha kufanya kazi za kila siku kwa urahisi.
  Uzuri
  Nyembamba, maridadi, nyepesi
  VivoBook Flip 14 ina fremu ya alumini inayovutia macho. Ikiwa na umbo la 19.2mm na uzito wa jumla ya 1.6kg, ni moja kati ya kompyuta pakato za inchi-14 zinazoweza kubadiliwa zilizopo.
  Muundo wa Alumini
  Umbo la 19.2 mm
  Kioo
  Kioo Onyeshi cha NanoEdge
  Kuweka kioo onyeshi cha inchi 14 cha HD Kamili kwenye fremu inayolingana na ya kompyuta pakato ya inchi 13 siyo rahisi — lakini NanoEdge bezel nyembamba sana ya 8mm ilifanya hili liwezekane. Muundo wa NanoEdge ni nini, VivoBook 14 ina uwiano wa kushangaza wa 78.7% wa kioo hadi kwenye kiunzi na eneo kubwa la kioo onyeshi kwa ajili ya utazamaji mzuri.

  Kioo onyeshi cha HD Kamili kina nyuzi 178˚ za teknolojia ya mwonekano mpana ili kuhakikisha rangi na uangavu vinakuwa halisi na kuonekana vizuri, hata vinapotazama kupitia kona kali. Hili linaifanya kuwa suluhisho kamili la kushirikisha maudhui kwa marafiki pamoja na wenzako.
  Paneli ya 14''
  Bezel nyembamba ya 8 mm
  Uwiano wa Kioo hadi kwenye Kiunzi 78.7 %
  HD Kamili 1920X1080
  Teknolojia ya Mwonekano Mpana 178˚
  Kioo cha Kugusa
  Mguso sahihi sana
  VivoBook Flip 14 imeundwa kwa ajili ya kuwa na mguso madhubuti. Vitambuzi vyake vyenye usahihi mkubwa vimewekwa kwa umbali wa uwiano wa 6mm ili kuhakikisha vinahisi vyema kuliko vile vya vioo onyeshi vya kawaida — kwa hiyo hata miguso midogo hutambuliwa.

  VivoBook Flip 14 pia inafanya kazi kikamilifu na kalamu ya ASUS.
  Kufahamu zaidi juu ya kalamu ya ASUS, tafadhali tembelea: https://www.asus.com/Notebooks-Accessory/Asus-Pen/
  Sauti
  SonicMaster - iliyoundwa kwa ajili ya sauti ya kushangaza
  Sauti halisi inayofanya burudani kuwa kubwa zaidi. Teknolojia ya ASUS SonicMaster - iliyoandaliwa na timu ya ASUS Golden Ear na ICEpower® - hutoa sauti ya kushangaza ambayo hujawahi kuisikia kwenye kompyuta pakato, hii inatokana na muunganiko wa kibunifu kati ya vifaa na programu.
  Utendaji
  Ipeleke-popote
  utendaji na ufanisi
  Ikiwa na hadi processor ya kizazi cha 7 ya Intel Core i7 na hazina data ya 16GB, VivoBook Flip 14 inatoa utendaji wenye nguvu, na unaookoa nishati. Ikiwa na hadi HDD ya 1TB na hifadhi data ya SSD yenye 256GB, VivoBook Flip 14 ina nafasi zaidi ya inayotoshwa kwa ajili ya uwasilishaji wa biashara yako, pamoja na maswala yote ya picha na video. Ukiwa ndani ya nyumba, au nje- utafanya zaidi na VivoBook Flip 14.
  WINDOWS 10 Pro
  Hadi Core i7 Intel CPU
  16 GB DDR4 2133MHz Yenye kasi
  Hadi 256 GB SSD
  Hadi 1 TB HDD
  Betri
  Tija ya siku nzima na burudani
  Ikiwa imejaa chaji, VivoBook Flip inaweza kudumu kwa siku nzima, kwa hiyo hutahangaika kutafuta mahali pa kuchajia. Na wakati wa kuiweka kwenye umeme, teknolojia ya kuchaji betri ya ASUS husaidia kulinda betri yako.

  Kuzidisha kuchaji betri ya kompyuta pakato yako kunaweza kupunguza maisha ya betri yako, au kuifanya ivimbe kutokana na oksidi. Teknolojia ya kuchaji Betri ya ASUS inayolinda afya ya betri hukuruhusu kuweka hali ya chaji kuwa 60%, 80% au 100% ili kuongeza maisha ya betri na kupunguza uwezekano wa uharibifu kutokana na betri kuvimba.
  Muunganisho
  Muunganisho wa uhakika wa wireless
  VivoBook Flip 14 ina Bluetooth® ya karibuni ambayo inaokoa nishati na Wi-Fi ya dual-band ya 802.11ac, ambayo inaaminika zaidi kwa kasi ya hadi 6X zaidi kuliko ya kizazi kilichopita cha 802.11n.
  Dual Band 802.11ac
  Uzuri
  Bawaba inayodumu
  Ili kuhakikisha inadumu kwa muda mrefu, bawaba ya chuma iliyotengenezwa vyema inayozunguka nyuzi 360 ° ya VivoBook Flip 14 ilijaribiwa kwa kufunguliwa na kufungwa mara 20,000 ili kuona ubora wake. Kwa hiyo unaweza kuwa na uhakika kuwa VivoBook Flip 14 yako itakuwa tayari kwa mkao wowote, kwa wakati wowote — kwa miaka mingi jayo!
  Bawaba yenye Nguvu 360
  Bawaba imejaribiwa mara 20,000
  Kugusa
  Andika kwa raha.
  VivoBook Flip 14 imetengenezewa kibodi nzuri sana yenye vitufe vyenye ukubwa kamili, na vyenye mwachano sahihi wa vitufe ili kukupa uhuru wakati wakuandika, hatakama unaandika kwa kasi kubwa. Vitufe vilivyotengenezwa kwa mfumo mzuri — vitufe vyenye taa ambavyo mwanga wake unaweza kutawaliwa, kwa hiyo utakuwa mwenye tija hata kwenye mazingira yenye giza — sifa kama hizi ndizo uitenga Flip TP410 kutoka kwenye kundi la kompyuta nyingine.
  Kibodi yenye Taa
  Ufikiaji wa mguso-mmoja
  kwa Windows Hello
  Kufikia VivoBook Flip 14 haijawahi kuwa rahisi au salama zaidi. Ikiwa na tachipadi iliyojumuishwa na kihisi alama za vidole pamoja na Windows Hello, siku za kuandika nywila zimekwisha — kuweka kidole mara moja tu kunatosha kukuruhusu kuingia!
  Kihisi Alama za Vidole
  Muunganisho
  Kwa uwezekano usio na kikomo
  Wakati wa kufanya kazi au kusafiri, uunganisho ni muhimu! VivoBook Flip 14 ina tundu la kimapinduzi la USB Aina-C ™ kwamuunganisho wowote na kuhamisha data kwa kasi kubwa.
  Kwa urahisi na utangamano, VivoBook Flip 14 ina uunganisho kamili ikiwa ni pamoja na tundu moja la 3.0, matundu mawili ya USB 2.0 2.0 za kawaida na HDMI ya kuunganisha vifaa mbalimbali vya ziada.
  Kadi ya SD X 1
  USB CX 1
  USB 2.0 X 2
  USB 3.0 X 1
  HDMI X 1
  Kugusa
  Kifikirie, kiandike!
  Kalamu ya ASUS inaweza kubaini migandamizo midogo kuanzia 10g hadi 300g. Inazidi kiwango cha wastani cha usahihi cha tasnia husika, nakuruhusu kuishika kwa kona za hadi nyuzi 45°, kama unavyoweza kufanya kwa kalamu ya kawaida.

  Andika mawazo yako, onyesha michoro, au bainisha mawazo yako — kalamu yenye usahihi sana na inayokupa utawala halisi, hukufanya ujisikie huru.
  Kiwango cha Mgandamizo 1024
  Nguvu ya Kichwa cha Kalamu 10-300 g