ASUS recommends Windows 10 Pro.

  ASUS VivoBook Flip TP501UA

  Geuza njia yako ya kazi na ya kucheza!
  Geuza njia yako ya kazi na ya kucheza!
  Uzito Mzuri 2.2 kg
  Nyembamba sana 22.5 mm
  Kompyuta Pakato Kamili kwa Ajili ya Tukio Lolote

  Kwa kupunguza kwa makini kila gramu ya mwisho, tumefanya VivoBook Flip TP501 ya inchi 15.6 kuwa nyepesi sana na kuwa na 2.2kg, ikiwa na umbo jembamba la 22.5mm. Yote haya hayafanyi tu Flip TP501 kuwa chaguo zuri kwa matumizi ya nyumbani au ofisini, lakini pia kifaa kamili cha kwenda nacho popote kinachokuwezesha kufanya kazi na kupumzika wakati wowote, popote pale.

  Umaliziaji wake bora wa chuma huifanya iwe na mguso unaovutia, na mwonekano wake maridadi huitofautisha na nyingine. Kwa kifupi, Flip TP501 inashangaza sana.

  Uhandisi imara, kutoka kila pembe

  Bawaba yenye nguvu ya kushangaza yenye nyuzi 360 ya Flip TP501, hukupa uhuru wa kupangilia maisha yako kwa njia unayoitaka. Fanya kazi kubwa kwenye modi ya kompyuta pakato. Ikunje kuwa kwenye modi ya hema ili kushirikisha au kujadiliana mambo na wenzako. Unda ukumbi wako binafsi wa sinema papo hapo kwa kupitia modi ya kusimama.

  Na popote ulipo, modi ya tableti ya Flip imeboreshwa kwa muundo mwepesi na maisha marefu ya betri.

  Bawaba yenye Nguvu 360
  Majaribio ya Bawaba 20,000
  Muunganiko wa Nguvu na Ufanisi
  Windows 10 Home
  HADI i7 Intel-core CPU
  HADI 940 M ya Picha za NVIDIA

  Flip TP501 inakupa utendaji wenye nguvu, wenye ufanisi wa nishati processor ya karibuni wa Intel® Core ™ i7 na picha za NVIDIA® GeForce ™ zenye ubora wa hali ya juu.

  Windows 10 pia inakuwezesha kufanya kazi kwa unadhifu na ulaini, na modi ya Continuum ambayo hubadilisha mpangilio wa kioo onyeshi cha Windows kulingana na jinsi unavyotumia Flip TP501 — kwa hiyo utaweza kupata utumizi bora zaidi wa Windows, kwa kila modi ya Flip!

  Uunganishwa kwa USB Aina-C na Wi-Fi ya 802.11ac
  Tundu jipya linalopindulika la USB Aina-C linarahisisha uunganishaji wa vifaa kwa kutumia USB 3.1 Gen 1 yenye kasi kubwa (hadi 5Gbit/s) ambayo hukuwezesha kuhamisha filamu ya 2GB kwenda kwenye drive ya USB kwa muda wa chini ya sekunde 2! Kwa ajili ya uhakika na utangamano mkubwa, TP501 pia ina USB 3.0 ya kawaida na matundu ya USB 2.0, pamoja na tundu la HDMI kwa ajili ya kuunganisha vifaa mbalimbali.
  Aina-C
  USB 3.0
  USB 2.0
  HDMI
  Kadi ya SD
  Wi-Fi ya 802.11ac inakupa matumizi bora ya mtandao - ikiwa na mawimbi yenye nguvu, imara zaidi na kasi ya kuhamisha data ambayo ni mara tatu ya kasi ya vizazi vya zamani vya Wi-Fi.
  Muunganisho wa juu wa Wi-Fi 802.11 ac
  Picha na sauti zenye uhalisia
  Flip TP501 hukupa picha zisizo na chenga na sauti inayosikika kikamilifu. Kioo onyeshi chake cha HD Kamili hukupa pembe pana za utazamaji, kwa hiyo picha hazitaonekana kuchuja au kukosa uangavu, hata kama unazitazama kwa pembeni. Hii inaifanya Flip TP501 kuwa bora kwa ajili ya kuwa skrini ya kushirikisha maudhui kwa kikundi cha watu, kwa kutumia modi yoyote ya Flip.
  Teknolojia ya kipekee ya ASUS SonicMaster inajumuisha vifaa vilivyotengenezwa vyema pamoja na marekebisho ya programu ili kutoa sauti halisi.
  Mrejesho wa Papohapo kwa Mguso Mwepesi
  Flip TP501 imeundwa kutoa mrejesho mara moja kwa kila mguso wako. Tumeongeza uwezo wa kuhisi mara mbili, kwa hiyo hata mijongeo midogo ya vidole itabainika, na inahitaji miguso laini sana pekee ili kufanya kazi vyema. Kwa hakika, ni nzuri sana kwani inatenda kwa usahihi hata kwa miguso midogo ya vidole kama ya mtoto!
  Inahisi mara 2 x
  Miguso Mingi ya Vidole Ipatayo 10
  Uhuru wa Kuandika Ndicho Kilichoko Kwenye Maelezo
  Kwa sababu tu Flip TP501 ya inchi 15.4 ni nyembamba sana, nyepesi na imara haimaanishi kuwa unapaswa kuteseka katika kuitumia kuandika. Tumetengeneza kibodi nzuri sana yenye vitufe vyenye ukubwa kamili, na vyenye mwachano sahihi wa vitufe ili kukupa uhuru wakati wakuandika, hatakama unaandika kwa kasi kubwa.
  Muundo imara wenye mkato wa mkasi
  Mwachano wa 1.6 mm
  Tachipadi sikivu ambayo ni maizi.
  Tachipadi kubwa kwenye Flip TP501 inakurahisishia kuvinjari kwenye Windows. Tumeifanya kuwa na uwezo mkubwa wa kuhisi ili itoe mrejesho wa papohapo, na kuondoa kuruka kwa mshale wa kipanya kunakokera pale kiganja kinapogusa tachipadi, tunatumia kanuni za kipekee ili kutambua tofauti kati ya kidole na kiganja. Ni usawa kamili kati ya kuhisi na utumivu.