ASUS recommends Windows 10 Pro.

  ASUS VivoBook Flip TP501UA

  Rudi juu
  Nguvu ya Utendaji ya Kizazi Kijacho
  Inaendeshwa na processor ya kizazi cha 6 ya Intel® Core ™ i7 ya hivi karibuni, VivoBook Flip TP501 inakupa utendaji wa daraja la kwanza, kwa kazi na kwa kucheza. Chip hii ya hivi karibuni ni nyembamba kuliko za awali – inakidhi kompyuta pakato ndogo. Usanifu uliotumia Skylake hutoa utendaji mzuri ili kuleta tija na uokoaji wa nishati wa kipekee. Matokeo ni kuchochea utendaji wa vifaa kwa ajili ya kucheza video, picha na sauti, uhariri wa haraka wa picha pamoja na uchakataji wa video wenye kasi kubwa. Kuongezeka kwa ufanisi wa matumizi ya nishati inamaanisha maisha marefu ya betri – hasa ni muhimu kwa matumizi ya kila siku!
  Ufanisi wa Utendaji wa Picha
  kwa ajili ya Burudani
  Flip TP501 inajumuisha processor ya picha ya NVIDIA® GeForce® 940M kwa ajili ya utendaji bora wa picha, sauti na video. Ufanisi wa picha ni wa kasi ya hadi mara tatu — hivyo unaweza kufurahia kikamilifu picha na video zako, peruzi mtandao, au cheza michezo yenye mipangilio onyeshi mikubwa. Processor ya graphics inaufanisi wa nishati, hii huongeza muda wa maisha ya betri ili kukupa muda zaidi wa kujifurahisha.
  Muunganisho Rahisi
  Flip TP501 inajumuisha tundu la hivi karibuni la USB Aina C, ambalo lina muundo unaopindulika kwa ajili ya miunganisho ya haraka na rahisi — hakuna kazi ya kubahatisha tena! Na ikiwa na USB 3.1 Gen 1, utaokoa muda kwa uhamishaji wa data wenye kasi kubwa unaofikia kasi ya mara 10 zaidi kuliko ya USB 2.0.
  Utumizi mzuri na Wenye Kasi wa Mtandaoni
  Wi-Fi ya 802.11ac inakupa utumizi bora zaidi wa mtandaoni - mawasiliano imara yenye nguvu, na kasi ya kuhamisha data ambayo ni mara tatu zaidi ya vizazi vya Wi-Fi vilivyopita. Wi-Fi ya zamani 802.11n inategemea njia za 40MHz ambazo zinaweza kuathirika kwa urahisi kwa kuingiliwa na simu za mkononi, Bluetooth, na vifaa vingine vya wireless vinavyotumia bandwidth sawa na 2.4GHz. Kizazi cha hivi karibuni cha Wi-Fi ya 802.11ac kinafanya kazi kwa bendi 5GHz na 80MHz kwa uimara zaidi na bila kuingiliwa kwa urahisi – kwa hiyo unaweza kustrimu maudhui ya HD Kamili au 4K/UHD bila tatizo.

  Vihisi Vingi Zaidi kwa Ajili ya Kuhisi Mguso Bora
  Kwa ajili ya usahihi na kuhisi kwa kipekee kwa skrini ya kugusa, Flip TP501 inatumia vihisi vyenye usahihi wa hali ya juu vilivyowekwa kwa uwiano wa 5mm, ambavyo ni karibu nusu ya kipimo cha wastani cha tasnia husika ambacho ni 9mm. Ikiwa na vihisi zaidi kwa sentimita ya mraba, Flip TP501 inafanya kila unachoiamuru - kila wakati!
  ASUS Flip TP501
  Kioo Kingine cha Kugusa
  Vihisi Mguso
  Nguvu
  Furahia kugusa kwingi kulikodhibitiwa vyema
  Kioo onyeshi cha maeneo 10 ya kugusa cha TP501’ kinakupa uwezo wa kutumia vidole vingi kwa usahihi na ukamilifu, inafaa sana kwenye modi ya kompyuta pakato, na hata kufaa zaidi kwenye modi ya tableti — kwa hakika, ni bora kuliko tableti ya kawaida
  Fanya Kazi Kimaridadi kwa Ishara Maridadi
  Teknolojia ya Ishara Maridadi ya ASUS inakuwezesha kutumia ishara za Windows za kisasa kwenye tachipadi kubwa, na kuifanya iwe rahisi zaidi kuvinjari au kutawala programu. Ishara Maridadi humudu hadi ishara za vidole vinne kwenye Windows 10, hivyo unaweza kubadili programu kwa urahisi, kufungua Cortana au Action Center kwa kugonga au kuswaipu kupitia skrini ya kugusa. Haijawahi kuwa rahisi kutumia tachipadi!

  Uzuri

  Kuswaipu kwa Upande wa Kulia

  Kuswaipu kwa Upande wa Kushoto

  Nenda kwenye App ya Mwisho

  Kupandisha na Kushusha Ukurasa wa Wavuti

  Juu na Chini

  Kukuza / Kupunguza

  Mfinyo wa Vidole Viwili

  Kugonga

  Kubofya-kulia

  Kubofya

  Kubofya-kushoto