ASUS recommends Windows 10 Pro.

  ASUS ZenBook Flip UX360CA

  Rudi juu
  ZenBook Flip inachanganya ufahari wa kisasa wa ZenBook na urahisi na ukubalifu wa kioo onyeshi kinachozunguka kwa 360°. Kompyuta pakato maridadi nyembamba sana, nyepesi sana inayoweza kubadiliwa, tableti inayobebeka, au kingine kinachofanana na hivyo — na imeundwa kuwa nawe kila mahali, wakati wowote. Programu yake ya Intel® Core inakuwezesha kufanya kazi zako za kompyuta za kila siku kwa urahisi, wakati betri yake ya kushangaza inadumu hadi saa 12 kabla ya kuichaji tena!
  Nyembamba, Maridadi na ya Kisasa.
  ZenBook Flip ni kito cha kifahari, kizuri kilichojengwa kutokana na alumini imara. Kiunzi chake kimeundwa kwa chuma kimoja, kimetengenezwa kwa umakini hadi kuwa na uwembamba wa 13.9mm, na uzito wa 1.3kg pekee ili kuifanya iwe rahisi kubebeka. Umaliziaji wake wa kipekee wa chuma, uliokamilishwa kwa upekee wa Zen, umewekewa rangi mbili za kipekee ili kukidhi mtindo wake ambazo ni : Icicle Gold ya kisasa au Mineral Grey maizi-sana.
    Nyembamba sana 13.9 mm
    Nyepesi Sana 1.3 kg
  Yenye Kupendeza Iliyohandisiwa Vyema.
  Ikijumuisha chuma kilichohandisiwa vyema, bawaba ya 360° kwenye ZenBook Flip, ina muundo madhubuti na utendaji bora ambao unashikilia kioo onyeshi kwa usalama kwenye kona yoyote. Ili kuhakikisha inaaminika, imejaribiwa vikali kwa mizunguko ya kufungwa na kufunguliwa zaidi ya mara 20,000, ili kuhakikisha unaweza kuibadili ZenBook Flip kwa urahisi kutoka kwenye kompyuta pakato ya utendaji wa juu hadi kuwa tableti nyepesi wakati wowote — bila tatizo!
    Bawaba yenye Nguvu 360
  Imejaribiwa vikali zaidi ya mara 20,000
  Rangi Inayofanana na Rangi Halisi, kutoka Kila Kona.
  Kuona ni kuamini. Skrini ya kugusa ina hadi muonekano wa QHD + 3200 x 1800 na mtandazo wa rangi wa 100% wa sRGB, ZenBook flip inakupa nelibini ya rangi ambayo ni wazi zaidi na sahihi. Ikiwa na ung'avu wa 350cd / m2, na kioo onyeshi chenye pembe pana ya kutazamia ya ubora wa hali ya juu, picha inakuwa kama picha halisi kwenye skrini, kutoka kila pembe.
  Mwonekano QHD+ hadi 3200X1800
    276 ppi  
    kioo onyeshi chenye mwonekano mpana wa 178
  Imejengwa kwa Ajili ya Watu wa Siku Nzima.
  ZenBook Flip UX360CA imetengenezwa kwa ajili ya kwendana na mtindo wa maisha uliosheheni mambo, ikiwa na processor inayookoa nishati ya Intel Core i7, betri yenye uwezo mkubwa ya lithiamu-polymer ambayo inaweza kudumu hadi saa 12 kabla ya kuichaji tena. Kwa hiyo hata kwenye safari ndefu za ndege, ZenBook Flip inaweza kumudu umbali huo kwa urahisi.
  Kasi ya Kushangaza, Ikiwa Kimya Kabisa.
  Vipengele bora pekee ndivyo vinavyofaa kwa ajili ya ZenBook Flip. Ikiwa na hadi RAM ya 8GB, SSD ya 512GB yenye kasi sana na processor ya karibuni ya kizazi cha 7 ya Intel Core i7, ZenBook Flip ina utendaji wa kumudu kazi yoyote ambayo unataka kuifanya - hata zaidi! Muundo wake bora usio na feni unamaanisha kuwa usumbufu ni mdogo: tumeihandisi ZenBook Flip kwa kutumia bomba za kupoozea ambazo ni nyembamba sana zenye kipenyo cha 0.5mm za aloi ya chromium-copper ambazo hukuwezesha kufanya mambo kwa utulivu, hata ukiwa kwenye utendaji kamili.
  WINDOWS 10 HOME
  Kihifadhi Data cha SSD 512 GB
  8 GB 1866 MHz RAM
  Intel Processor ya i7
  Kuunganishwa Kusikokuwa na Shida.
  Wakati wa kufanya kazi nyingi, ni muhimu kuweza kuunganisha na kitu chochote na kila kitu. VivoBook Flip ina tundu la kimapinduzi la USB Aina-C kwa ajili ya muunganisho wowote na kuhamisha data kwa kasi kubwa. Na utapata pia matundu mawili ya USB 3.0 Types-A, tundu la micro HDMI na sehemu ya Kadi ya SD, kwa hiyo ni rahisi kuunganisha vifaa vya sasa na vya baadaye.
  Micro HDMI
  USB Aina-C
  USB 3.0
  Wi-Fi yenye Kasi,
  Wi-Fi Bora.
  ZenBook Flip inakuja na Wi-Fi ya karibuni ya 802.11ac,. yenye kasi sana ya hadi 867Mbps. Ambayo ina kasi mara tatu zaidi kuliko vizazi vya zamani vya Wi-Fi, na ina mawimbi yenye nguvu, na imara zaidi. ZenBook Flip inamudu teknolojia ya Intel WiDi, ili uweze kustrimu muziki, sinema, picha na michezo kwenye HDTV yoyote inayomudu WiDi, au kutumia TV kama skrini ya pili ili kupata skrini kubwa kwa ajili ya kazi mbalimbali.
    Muunganisho wa juu wa Wi-Fi 802.11 ac
  Mguso, Umekamilishwa.
  ZenBook Flip imeundwa kwa ajili ya mguso wa kipekee, ikiwa na skrini ya kugusa yenye uwezo wa hali ya juu inayofanya ufurahie kuitumia kwenye modi yoyote. Vihisi vyake vinaweza kuhisi mguso kwenye eneo la 6mm — vinahisi zaidi kuliko kiwango cha wastani cha tasnia husika ambacho ni 9mm — kwa hiyo hata mijongeo midogo ya vidole itatambuliwa.
  Inahisi mara 2 x
  Miguso Mingi ya Vidole Ipatayo 10
  Andika kwa Raha.
  Kuandika hakutakiwi kuchoshe. Kibodi bora ya kipekee ya ZenBook Flip ni nzuri kwa ajili ya utendaji bora wa kazi kwa ajili ya kukupa uandishi mzuri, ikiwa na vitufe kamili vyenye mwachano ulioboreshwa wa 1.5mm kwa ajili ya uandishi huru kama wa kwenye deskitopu. Na unapoingia kwenye modi ya tableti, kibodi na tachipadi hujizima zenyewe moja kwa moja!
    Mwachano 1.5 mm
  Tachipadi Halisi na Sahihi.
  Tachipadi sahihi sana iliyoko kwenye ZenBook Flip ina teknolojia ya ASUS Smart Gesture kwa ajili ya mguso halisi, unaotumia vipengele vile vile vinavyotumiwa kwenye miguso ya Windows kwenye skrini ya kugusa. Tachipadi inatumia teknolojia ya kipekee iliyoundwa kwa ajili ya skrini za kugusa za simu za kisasa, hili huifanya ihisi kwa kiwango cha juu na kwa usahihi.
  SonicMaster, Iliyoundwa Kutoa Sauti ya Kipekee.
  Daima sauti ya kipekee imekuwa kipengele cha familia ya ZenBook. Imetengenezwa kwa ushirikiano wa timu ya ASUS Golden Ear na ICEpower®, teknolojia ya sauti ya ASUS SonicMaster hutoa sauti ya kipekee zaidi kwenye kompyuta pakato. Mchanganyiko unaojumuisha vifaa bora na programu zilizobuniwa vizuri huipa ZenBook Flip sauti bora sana.
  Uzoefu Bora wa Windows 10.
  Windows 10 ni mpya na iliyoboreshwa, lakini hufahamika kwa urahisi, hili huifanya kuwa chaguo kamili kwa ajili ya ZenBook Flip. Siyo tu rahisi sana kutumia, lakini kwa msaada wa Cortana — msaidizi wako binafsi mwenye akili — unaweza kuamka na kuanza kukimbia mara moja! Modi mpya ya Continuum kwenye Windows 10 huhama yenyewe kwa urahisi ili kukidhi namna unavyofanya kazi: Modi ya kompyuta pakato imeboreshwa kwa ajili ya kibodi na kipanya, na Modi ya tableti imeboreshwa kwa ajili ya kugusa, kwa hiyo kila wakati utafurahia matumizi yenye ubora wa hali ya juu.