ASUS recommends Windows 10 Pro.

  ASUS ZenBook Flip UX360CA

  Rudi juu
  Kung'aa Kulikotengenezwa-kikamilifu.
  ZenBook Flip ni kazi ya kisasa ya kisanaa, iliyotengenezwa kwa umakini kutoka kwenye umbo moja la chuma.Imeundwa ionekane ya kuvutia pia, ikiwa na sifa ndogo ndogo lakini muhimu kama vile kingo laini za uduara.Hatuchukui uchaguzi rahisi, pia: umaliziaji wa chuma maalumu unahitaji hatua 32 ili kukamilisha umaliziaji bora wa chuma cha Zen.Waundaji wetu hutilia maanani hata mambo madogo, kama vile mkato wa nyuzi 25° wa upande wa chini ya kifuniko ili kuifanya ZenBook Flip kuwa rahisi kufunguliwa.
  LAINI SANA
  Uso wa Kiwango cha 170-Zircon Sand-Blasted
  BAWABA ZA-UNI
  Carbon-Steel Aloi ya kipenyo cha 4.5mm
  ya Kiunzi iliyomaliziwa Vyema
  Swivel Iliyoimarishwa
  SAUTI ILIYOBORESHWA
  Inatoa 2x zaidi kuliko UX305
  Matundu ya micro-etched ya 1240 0.4mm
  KAZI KWENYE MFUMO
  Mkato wa Chini wa Nyuzi 25 Unafanya Kufungua
  Kuvutie na Kuwe Rahisi
  Maajabu ya Uhandisi.
  Kuweka bawaba ya 360 ° kwenye ZenBook haikuwa rahisi.Timu yetu ya uundaji na timu za uhandisi zilitumia muda mrefu kufahamu jinsi ya kupunguza ukubwa wa utendaji wake hadi kipenyo cha 4.5mm ili iingie kwenye umbo dogo sana.Lakini kama ilivyo siku zote, walifanikiwa.
  zaidi ya mara 20,000   Ilijaribiwa Vikali
    4.5 mm Kipenyo
  Kwa ajili ya uhakika mkubwa, bawaba zinatumia muundo wa umbo moja lililohandisiwa vyema kwa aloi ya carbon-steel.Kuhakikisha haikupi matatizo, tuliijaribu vikali kwa zaidi ya mizunguko 20,000 ya kufungua na kufunga.Matokeo yake ni kwamba unaweza kuibadili ZenBook Flip kwa urahisi kwenda kwenye modi yoyote unayotaka, wakati wowote - bila shida!
  Angalia Kila Kitu kwa Uwazi, Kila mahali
  Rangi Zaidi, Rangi Bora.
  Kioo onyeshi cha kiwango cha juu cha QHD + kwenye ZenBook Flip hutumia vifaa na programu bora ili kuunda kioo onyeshi bora zaidi.Ina mtandazo mpana wa kipekee wa rangi wa kiwango cha juu cha 72% ya NTSC, 100% sRGB na 74% ya Adobe RGB ambayo kwa lugha rahisi, ina maanisha inaweza kuonyesha rangi zaidi, rangi zenye muonekano wa asili zaidi na rangi kwa uwazi zaidi kuliko kioo onyeshi chochote cha kawaida.Mara tu baada ya kuizoea, hakuna kitu kingine kitakachotosha kuifikia.
  Kwa lugha rahisi, hii ina maana kuwa inaweza kuonyesha rangi zaidi, rangi sahihi zaidi na rangi zaidi kwa uwazi kuliko kioo onyeshi chochote cha kawaida.Mara tu baada ya kuizoea, hakuna kitu kingine kitakachotosha kuifikia.
    100 % sRGB
    178 Eneo pana la kutazama
    72 % NTSC
  Picha Bora, Daima.
  ASUS Mng'ao ni njia rahisi ya kudhibiti mipangilio ya kioo onyeshi.Ina modi nne rahisi zilizopo:Modi ya Kawaida, Modi inayolinda Macho, Modi dhahiri na Modi inayowekwa na mtumiaji.Modi ya kawaida inakupa mipangilio ya kiwandani iliyoboreshwa, Modi inayolinda macho hupunguza viwango vya mwanga wa bluu kwa 30% ili uone vizuri, na Modi dhahiri inawezesha mipangilio ya kioo onyeshi kutoa picha katika mwonekano halisi, bila kufanya rangi kuonekana siyo halisi.Modi inayowekwa na mtumiaji hukupa utawala juu ya mipangilio ya joto la rangi, kwa hiyo unaweza kubadilisha mpangilio wa kioo onyeshi ili kukidhi matakwa yako.
  Teknolojia ya ASUS Tru2Life
  Video ya Pixel-kamilifu.
  Video ya Pixel-kamilifu.
  Teknolojia ya video ya ASUS Tru2Life Video hufanya video zako zionekane za kushangaza.Inatumia kanuni mahiri za programu ili kuongeza ukali na uangavu wa kila pikseli kwenye kila fremu moja ya video — hiyo ni sawa na mahesabu milioni moja kwa sekunde — hivyo kila mara utafurahia picha bora kadri iwezekanavyo.