Kuhusu ASUS

  Ili kufikia lengo letu la kuifanya ASUS kuwa biashara ya kutamanika zaidi duniani kwenye zama za kidigitali; tunajiendesha kulingana na misingi minne ambayo inaunda DNA ya ASUS.

  Msingi wa kwanza kati ya minne unagawanywa katika manufaa matano ambayo tunaamini ni muhimu kwenye maendeleo thabiti ya michakato na mahusiano, na kila mtu anayefanya kazi ASUS anahimizwa kuifanya.

  Manufaa 5 ya ASUS

  ASUS inaweka umuhimu mkubwa juu ya manufaa ya mfanyakazi. Tabia tano zimebainishwa kama ufunguo wa maendeleo laini ya michakato na mahusiano. Manufaa matano ya ASUS ni:

  Unyenyekevu

  • Onyesha shukrani na heshima kwa wengine
  • Kuwa na roho kubwa ya kukaa kwenye timu
  • Unapokabiliwa na matatizo, angalia maeneo ya wajibu binafsi badala ya kulaumu wengine
  • Kuwa na motisha sana na jitahidi kujiboresha wewe binafsi

  Uadilifu

  • Kuwa mwaminifu, mwazi na mkweli
  • Elewa na kubali nguvu na udhaifu wa mtu mwingine
  • Endeleza uhusiano wazi wa kitaalamu

  Bidii

  • Endeleza uhusiano wazi wa kitaalamu
  • Zingatia gharama na ondoa upotevu kwa ‘kufanya zaidi kwa vichache’
  • Chukua hatua ya kuzileta timu za mradi pamoja ili kutengeneza kiwango cha juu cha thamani kwa mteja

  Wepesi

  • Kuwa mwepesi kuelewa misingi ya hali yoyote
  • Chukua hatua sahihi haraka ili kuunda matokeo bora
  • Tafuta na chukua fursa mpya haraka

  Ujasiri

  • Kabiliana na matatizo na kubali shida
  • Fanya majadiliano mazuri, hata kama unakabiliwa na kutokuelewana na upinzani
  • Zingatia ukweli uliopo kabla ya kutoa hitimisho ili kuepuka kufanya maamuzi ya ghafla

  Zingatia Misingi

  Ili kufikia matokeo bora kadri iwezekanavyo, kila mtu ndani ya ASUS anahimizwa kuzingatia misingi ya kazi kabla ya kuitekeleza.

  Kwa kuzingatia masuala mapana ya hali na kushughulikia matatizo kutoka kwenye mtazamo wa mteja muhimu, msingi huu husaidia kugundua utatuzi — wenye mafanikio — na wa gharama nafuu.

  Ubunifu na Uzuri

  Watu wote ndani ya ASUS wanajitahidi kuwa na ukamilifu wa teknolojia na uzuri katika kila kitu wanachofanya. Msingi huu unahusisha uchangiaji wa mawazo wa 'taa ya kijani', ambapo kila wazo hukusanywa pamoja na kisha suluhisho bora hutokana na mawazo hayo; wakati kufikiri kwa 'taa nyekundu' kunahusisha kuhoji mara kwa mara ili kuchuja matatizo yaliyotokana na kila pendekezo. Majaribio kama hayo husaidia kuendeleza bidhaa zinazozidi matarajio ya mteja na kuboresha uzoefu wa jumla wa bidhaa.

  Kufikiri kwa Lean

  ASUS inategemea 'kufikiri kwa lean' kuunda thamani kubwa kwa watumiaji kwa kuhamasisha mawasiliano ya wazi kati ya ngazi zote ndani ya shirika. Msingi huu unahusisha kanuni za Lean Six Sigma ili kuongeza ufanisi wa mchakato wowote, kupunguza gharama zisizokuwa za lazima na upotevu, na kuendelea kuboresha michakato ya usimamizi.