Kuhusu ASUS

  Kila bidhaa ya ASUS imekita mizizi yake kwenye muundo mzuri na ubunifu wetu wa kipekee na ukamilifu unaoanza kwenye kibao cha mchoro.

  Makao Makuu ya Uundaji ya ASUS yaliyoko Taipei yameundwa na wabunifu 100 kutoka sehemu mbali mbali ulimwenguni. Wakiwa wamegawanywa kwenye timu tisa, kila timu inahusika na maeneo kama vile uandaaji wa malighafi, usanifu wa mitambo na usanifu wa kiwandani.

  Bila kujali utaalamu wao, kila timu huweka jambo moja akilini — uzoefu wa mtumiaji. Kwa hakika muundo mzuri ni kuweka bidhaa kwenye mikono ya watu; bidhaa iliyofanikiwa ni ile ambayo kila mtu anapenda kuitumia.

  Msukumo wa Usanifu

  Bidhaa nyingi mpya hutengenezwa kwa kufuata lengo la ASUS, lakini msukumo kutoka kwa wengine hupelekea majadiliano ya mwaka ya usanifu wa ASUS.

  Theme zinazosaidia kuzalisha mawazo — ‘Kifahari’ theme ya 2006 ilipelekea utengenezaji wa kompyuta ya kushangaza ya kuchezea michezo ya kompyuta ya ASUS-Lamborghini, wakati 2007 theme ya ‘Kijani’ ilitoa hamasa ya Ess PC halisi.

  Ulimwengu wa usanifu kamwe hautulii, na bidhaa zetu hubadilika kila mara ili kutengeneza fursa mpya za masoko na kufikia mahitaji ya wateja yanayobadilika kila mara.

  Mwaka 2009, tulitazama wazo la zamani kuwa supercomputers zilipaswa ziwe kuwa sana kama kabati ambayo ilihitaji matengenezo ya kiwango cha juu na tukaunda ASUS ESC1000 — desktop supercomputer ya kwanza duniani.

  Ina uwezo wa 1.1 teraflops (Floating Point Operations trilioni 1.1 kwa sekunde), na kuifanya supercomputer kupatikana kwa mashirika yanayojiendesha kwa bajeti ndogo.

  Fahamu zaidi kwenye Tovuti ya Usanifu ya ASUS