Kuhusu ASUS

  Ubunifu wa kuvutia • Ukamilifu Endelevu

  Ubunifu wa Kuvutia • Ukamilifu Endelevu (UKUE) ni ahadi ya kampuni ya ASUS. Inaonyesha dhamira yetu ya kufanya maisha kuwa bora kwa njia ya uvumbuzi, na imani yetu kuwa mabadiliko ya maisha yanaweza kupatikana tu kwa kuendelea mbele ya mkondo na sio kupumzika kwenye mafanikio ya zamani.

  Ubunifu wa Kuvutia • Ukamilifu Endelevu sio tu usimamizi wa mumbo jumbo — ni falsafa inayoongoza ambayo inajitokeza kwa njia nyingi kwenye shirika la ASUS.

  Ubunifu wa Kuvutia — Ambapo Uwezekano wa Kushangaza Unaibuka

  'Ubunifu wa Kuvutia' ulianza nyuma tangu mwanzo mdogo wa ASUS mwaka 1989, ambapo hatua moja ndogo ilisababisha kusogea sehemu kubwa. Ubunifu wa Kuvutia ni imani imara kuwa mambo yanaweza kuboreshwa kila wakati. Ni uwezo wa kuangalia zaidi ya ufumbuzi unaojulikana na kuwa na ujasiri wa kutafuta kitu kipya, na inaelezea shauku ya kufanya ndoto za wateja wetu kuwa kweli kupitia ujuzi na kujitoa kwa ASUS.

  Ukamilifu Endelevu - Katika Ufuatiliaji wa Ubora

  Kila mfano wa uhandisi wa ASUS hupitia hatua thabiti za tathmini za kuhakikisha kwamba wazo linalopatikana linazidi matarajio ya mtu yeyote. Ikiwa ni usanifu au utendaji, kila kitu cha ASUS kilichokamilika kinajumuisha saa nyingi za kujitoa ili kuhakikisha kuwa lengo hili linatambulika. Ukamilifu Endelevu unajumuisha ahadi ndogo ya kukamilisha kuridhisha wateja, lakini inakwenda zaidi ya kutoa ufumbuzi kamili — ASUS inalenga kutoa uzoefu kamili.

  "Ubunifu wa Kuvutia • Ukamilifu Endelevu" ni kanuni yetu kwa ajili ya matarajio makubwa kwenye kila kitu tunachokifanya na kuhakikisha tunaridhisha wateja kila mara. Itakuwa ni chati ya ASUS ili kutimiza maono yetu ya kuwa biashara inayovutia sana inayoongoza katika zama mpya za digitali duniani, na itaendelea kutumika kama mpango wa kufanya ndoto za wateja wetu kuwa halisi kwa miaka mingi ijayo. "