Kuhusu ASUS

  ASUS, muuzaji wa 3 wa juu duniani wa notebook na mtengenezaji wa motherboard zinazouzwa zaidi duniani na zenye tuzo nyingi zaidi, ni kampuni inayoongoza kwenye zama mpya ya kidigitali. ASUS inabuni na kuzalisha bidhaa ambazo zinakidhi kikamilifu mahitaji ya nyumba ya leo ya kidigitali, ofisi na mtu binafsi, ikiwa na mkusanyiko mpana unaojumuisha motherboard, kadi za picha, optical drives, vioo onyeshi, desktopu, Eee Box na all-in-one PC, notebook, tableti, seva, multimedia na vifaa vya wireless, vifaa vya mitandao, na simu za mkononi. Ikiendeshwa na uvumbuzi na kujitolea kwenye ubora, ASUS ilishinda tuzo 3,886 mwaka 2011, na inajulikana sana kwa kuleta mapinduzi ya sekta ya kompyuta (PC) kupitia Eee PC ™. Ina wafanyakazi wa kimataifa zaidi ya 11,000 na timu bora kabisa duniani ya wahandisi ya R & D 3,000, mapato ya kampuni kwa mwaka 2011 yalikuwa karibu Dola za Marekani bilioni 11.9.

  Ikiongozwa na mahitaji mbalimbali ya watumiaji katika maeneo yote na hatua za maisha, jukumu kuu la ASUS ni kutoa ufumbuzi wa kibunifu wa kweli ambao huwahimiza watumiaji kufikia viwango vya juu vya uzalishaji na furaha. Kwa kuzingatia uelewa wa karibu wa mahitaji ya nyumba ya kisasa ya kidigitali, ofisi ya kidigitali na mtu wa kidigitali, ASUS inastahili heshima ya kudai kuwa ya kwanza duniani—kama vile kuanzishwa kwa Eee PC ™ ya kipekee, kutumiwa kwa ufanisi kwa vifaa vinavyoweza kutumika tena kama vile ngozi na mianzi katika notebook na kuingizwa kwa teknolojia ya injini ya Super Hybrid inayookoa nishati katika notebook zake na motherboard.

  Ubunifu ni msingi wa mafanikio ya ASUS. Kwa kuzindua PadFone kwa hadhira ya rapturous kwenye Computex 2011, mwaka huu Mwenyekiti wa ASUS Jonney Shih aliongeza kiwango cha mafanikio zaidi kwa tangazo la TAICHI na Transformer book-simu zenye matumizi zaidi ya moja.

  ASUS TAICHI ni Ultrabook yenye kuonyesha mara mbili ambayo inaruhusu itumike kama tableti wakati kifuniko kimefungwa, wakati Transformer Book ni tableti ambayo inaweza kufungwa kwenye kibodi kwa ajili ya mabadiliko ya papo hapo kuwa Ultrabook.

  Pamoja na Tableti ya 810 yenye Windows 8 na Tableti ya 600 yenye Windows RT, ASUS ina safu ya bidhaa ambazo zitazidi mawazo ya watumiaji wake wakati ulimwengu unapoingia kwenye zama mpya ya kompyuta mtandao.

  Kwa kuanzisha uvumbuzi mpya, mwenendo na teknolojia ambazo zimekuwa na matokeo halisi kwenye maisha ya wateja wake na Dunia kwa ujumla, ASUS inatarajia kukubalika zaidi kwenye fikra za watumiaji pamoja na kwenye soko.

  Ili kufanikiwa katika sekta ya TEHAMA yenye ushindani mkubwa, ASUS inalenga kasi ya kuingia sokoni, gharama na huduma. Ndiyo maana kila mfanyakazi wa ASUS anajitahidi kupata "ASUS Njia ya Usimamizi wa Ubora wa Jumla" ili kutimiza ahadi ya kampuni ya “Uendelevu Kamilifu”. Kwa Kuongozwa na maagizo haya, ASUS imetumia jitihada kubwa katika kubuni bidhaa, teknolojia, ubora na thamani / gharama. Jitihada hizi kwa upande wake huunda kanuni ya ASUS ya mafanikio—ikiruhusu uuzaji kuwasilisha faida hizi ili kuridhisha mioyo ya watumiaji wetu.

  Maono ya Kampuni

  ASUS daima hujitahidi kuwa mtoaji wa suluhisho wa C3 (Kompyuta, Mawasiliano, vifaa vya kielektroniki — Computer, Communications, Consumer electronics ) ambavyo hutoa ubunifu ambao unarahisisha maisha ya wateja wetu na kuwawezesha kutambua uwezo wao wote. Bidhaa za ASUS zinawakilisha kile bora ambacho teknolojia inatakiwa kutoa, zikitoa utendaji bora na uzuri wa kupendeza ambao humudu mitindo yote ya maisha, wakati wowote, mahali popote.

  Dhamira na Falsafa

  Kama mhusika mkubwa katika sekta ya TEHAMA, dhamira ya shirika la ASUS ni kutoa ufumbuzi wa kibunifu wa TEHAMA ambao unawawezesha watu na biashara kufikia uwezo wao wote. Falsafa ya ASUS iliyo nyuma ya utengenezaji wa bidhaa—ambayo ni kukamilisha misingi ya kwanza vizuri kabla ya kusonga mbele—imesababisha kupatikana kwa vifaa vinavyotegemewa vya uti wa mgongo wa kompyuta kama vile motherboards, kadi za picha, na vifaa vya uhifadhi wa data. ASUS sasa ina zaidi ya jamii 16 za bidhaa, ikiwa ni pamoja na bidhaa zake zinazoleta mabadiliko kwenye sekta husika za Eee na Transformer, mifumo ya wazi ya desktopu, seva, notebooks, vifaa vya mkononi, vifaa vya mtandao, mawasiliano ya broadband, vioo onyeshi vya LCD, TV, programu za wireless, na bidhaa za CPT (chassis, power supply and thermal).

  Kukamilisha Dhamira Yetu

  ASUS ina mpango wa kufikia dhamira yake kupitia Nia ya Teknolojia, Ikizingatia Ubora, Uhusiano wa muda mrefu, na Uvumilivu

  Shauku kwa ajili ya Teknolojia

  Teknolojia ni moyo wa ASUS. Tunaendelea kuwekeza katika Utafiti wetu na Maendeleo bora duniani ili daima tuweze kutoa ubunifu unaoongoza kwa watu na biashara.

  Kuzingatia Ubora

  Ubora ni muhimu sana kwa ASUS. Tunaendelea kuboresha michakato yetu ya usimamizi wa ubora ili kuhakikisha wateja wanapata ufumbuzi wenye ubora wa juu zaidi kwa gharama nafuu.

  Uhusiano wa muda mrefu

  Ikiwa ni wateja wetu, vyombo vya habari, wanahisa au watumiaji, tunaamini kukua pamoja na washirika wetu katika ngazi zote. Kudumisha uhusiano mzuri na wadau muhimu ni moja ya mambo muhimu zaidi ya muendelezo wa mafanikio yetu.

  Uvumilivu

  Waajiriwa wote wa ASUS hushiriki maana ile ile ya lengo. Sisi hustawi chini ya shinikizo na kuangalia mbele kwenye changamoto. Tunafanya kazi ili kukamilisha dhamira ile ile — kuwawezesha watu kupitia ufumbuzi wa kibunifu wa TEHAMA.

  Falsafa ya Usimamizi

  • Kuhamasisha, kuhimiza na kulea wafanyakazi wetu kufikia uwezo wao wa juu
  • Kujitoa kwa uadilifu na bidii; kuzingatia misingi na matokeo
  • Kuendelea kusikokoma kushindania namba 1 katika maeneo ya ubora, kasi, huduma, ubunifu na gharama nafuu
  • Kujitahidi kuwa miongoni mwa viongozi wa kimataifa wa teknolojia ya hali ya juu na kutoa michango ya thamani kwa binadamu