ASUS recommends Windows 10 Pro.

  ASUS ZenBook UX310UA

  Rudi juu
  Nyororo Sana. Utendaji Usiosimama.
  Nyororo Sana. Utendaji Usiosimama.
  ZenBook mpya ya UX310 inakupa umaridadi, ukisasa na utendaji mzuri wa kipekee katika muundo mwembamba na mwepesi wa kupendeza. Imetengenezwa kutokana na alumini imara na kukamilishwa kwa kutumia chuma cha kipeekee cha Zen, ZenBook UX310 inauwembamba wa 18.35mm tu. Na uzito wake rafiki kwa ajili ya safari wa 1.4kg unaamaanisha kuwa haitakuwa mzigo kwako kuibeba, na kuitumia kutakuwa starehe kwa uthabiti wake, ikiwa na kioo onyeshi angavu chenye ukubwa wa 13.3 inch. Ikiwa imejumuisha Intel® Core™ processors za kizazi cha nane, hazina data zenye kasi kubwa, ZenBook UX310 haiendi kwa kujikokota, hata hivyo — ina utendaji wote unaouhitaji katika siku yako ya kazi. ZenBook UX310 inafanya kila kitu kuwa rahisi, kwa mtindo.
  Nyororo Sana. Kifahari Sana
  Matoleo ya ZenBook hutengenezwa kwa kuzingatia uwembamba na uwepesi, na ZenBook UX310 imeendeleza urithi huo wa kujivunia, ikijumuisha muundo mpya wa kifahari wenye umbo la upana wa 18.35mm tu. Kutumia alumini imaara ya aloi kumefanya uzito kupungua hadi 1.4kg, lakini iligharimu hatua nyingi za utengenezaji zilizohusisha uangalizi wa karibu ili kuifanya kuwa na umbo nyororo. Umaliziaji wetu wa chuma, wenye chuma cha Zen, ulipamba kifuniko, huku ukihusisha umaliziaji kwa chuma kigumu na kinachodumu kilichosuguliwa kikipamba sehemu nyingine zilizobakia. Hatimaye, tukaifunika ZenBook UX310 kwa rangi ambazo zinahusiana na asili: Grey Quartz au Gold Gold.
    Nyepesi Sana 1.4 kg
    Nyembamba sana 18.35 mm
  Utendaji
  Utendaji wa Ajabu
  Utendaji bora ni sifa bainifu ya ZenBook, na katika ZenBook UX310 hili linaletwa na Intel® Core ™ hadi i7 processor ya kizazi cha 8, ikiwa na RAM yenye ukubwa wa hadi 16GB DDR4 2133MHz kwa ajili ya video nzuri ya kipekee. Bendi ya Wi-Fi ya 802.11ac ya hivi karibuni inakupa kasi kubwa sana, na Bluetooth® 4.1 ni rahisi kuunganishwa na vifaa vyako. Wataalamu wa kweli wanataka teknolojia ya kisasa, na kileta mapinduzi, tundu la USB Aina-C linalopindulika linakupa uwezo wa kuvifikia kwa kasi kubwa vifaa vya kisasa vyenye utendaji mkubwa. Kupitia tundu la HDMI, unaweza kuunganisha monita, TV au projekta bila tatizo. Kufanya kazi nyingi kwa pamoja bila shida, kucheza video kwa urahisi, na kufungua programu kwa haraka sana — ZenBook UX310 iko tayari kila mara unapoihitaji. Pia ina ufanisi mkubwa wa matumizi ya nishati, inamaanisha safari chache kwenda kwenye soketi ya umeme!
  WINDOWS 10 PRO
  hadi Core i7 Intel CPU
  hadi 16 GB DDR4 RAM
  kasi kubwa 2133 MHz RAM
  Kioo Onyeshi
  Kila Taarifa Inaumuhimu.
  hadi 3200X1800 Mwonekano QHD+
    276 ppi 
  Kioo onyeshi kinachoshangaza chenye hadi QHD+ (3200x1800) 13.3-inchi kinakufanya uone vizuri, ikiwa unasoma maandishi, unatazama picha au unatazama video. Mwonekano wa kushangaza unafanya uhariri wa picha au video kuwa rahisi, ikiwa na mshindilio wa kushangaza wa pikseli wa 276 kwa inchi, huu ni mdogo sana ambao unafanya kitu kionekane vyema sana. Na unapokuwa unaperuzi mtandao, kila kitu-hata kama ni maandishi madogo sana - yanaonekana kwa urahisi!
  Rangi Nyingi Zaidi. Rangi Bora.
  Kioo onyeshi cha ZenBook UX310 kinahusisha upana wa kipekee wa rangi wa 72% ya NTSC, 100% sRGB, na 74% ya AdobeRGB. Kwa lugha rahisi, hii ina maana kuwa inaweza kuonyesha rangi zaidi, rangi sahihi zaidi na rangi zaidi kwa uwazi kuliko kioo onyeshi chochote cha kawaida. Na teknolojia ya mwonekano mpana inahakikisha kuwa uzalishaji wa uangavu na rangi haupungui hadi digrii 178° , ZenBook UX310 huweka kiwango cha wastani cha vioo onyeshi vya kopyuta pakato.
    72 % NTSC
    100 % sRGB
    Kioo Onyeshi Chenye Mwonekano Mpana wa 178
  Mng'ao wa ASUS:
  Rangi Iliyoboreshwa Sana.
  Ili kuhakikisha upatikanaji wa picha bora zaidi pekee, ZenBook UX310 inatumia teknolojia ya Mng'ao ya ASUS ili kukupa rangi zilizojaa, zilizokolea, na sahihi zaidi.

  ASUS Mng'ao ina modi nne zinazoweza kubadiliwa kwa kubofya mara moja: Modi ya Kawaida, Modi inayolinda Macho, Modi dhahiri na Modi inayowekwa na mtumiaji. Modi ya kawaida inakupa mipangilio ya kiwandani iliyoboreshwa, Modi inayolinda macho hupunguza viwango vya mwanga wa bluu ili uone vizuri, na Modi dhahiri inawezesha mipangilio ya kioo onyeshi kutoa picha katika mwonekano halisi, bila kufanya rangi kuonekana siyo halisi. Modi inayowekwa na mtumiaji hukupa utawala juu ya mipangilio ya joto la rangi, kwa hiyo unaweza kubadilisha mpangilio wa kioo onyeshi ili kukidhi matakwa yako.
  Linda Macho Yako kwa Kutumia Modi Inayolinda Macho ya ASUS
  Kukaa kwa muda mrefu kwenye mwanga wa bluu unaotolewa na vioo onyeshi vya LCD kunaaminiwa kuathiri afya ya macho, inaweza kusababisha uchovu endelevu katika vipindi vya kutazama vioo hivyo kwa muda mrefu. Modi ya Kulinda Macho ya ASUS inapunguza utoaji wa mwanga wa bluu kwa zaidi ya 30% kwa hiyo kila mara macho yako yamelindwa wakati ambapo Modi ya Kulinda Macho inapotumika.
  Mfumo wa Kulinda Macho
  / Zima
  Mfumo wa Kulinda Macho
  / Washa
  Uwezo wa Juu wa Kihifadhi Data.
  Kasi kubwa ya kihifadhi data ni muhimu sana kwa ajili ya programu kufunguka kwa kasi na matumizi ya kompyuta yasiyokuwa na matatizo, ZenBook UX310 inakuja na hard disk (HDD) yenye kasi hadi 1TB ikijumuishwa na Solid state disk (SSD) . Kuhifadhi au kufungua faili ni haraka sana ukilinganisha na hard disks za kawaida, na muda wa kopyuta wa kuwaka umepunguzwa kwa kiasi fulani. SSD ni ngumu na zinadumu pia, hili huifanya ZenBook UX310 iaminike sana.
    1 TB HDD
    +    
    512 GB SSD
  Muunganisho wa Kipekee
  ZenBook UX310 ina tundu jipya linalopindulika la USB Aina-C lililotengenezwa kawa njia ambayo inafanya uunganishaji wa vifaa kuwa rahisi zaidi. Pia hutoa kasi ya uhamishaji wa data wa hadi mara 10 kwa kasi zaidi kuliko viunganisho vya zamani vya USB 2.0!

  Zaidi ya hayo, ZenBook UX310 ina matundu ya USB 3.0, tundu la HDMI na sehemu ya kuweka Kadi ya SD ili uweze kuunganisha kwa urahisi vifaa vyako vya sasa, vioo onyeshi na projekta bila tatizo lolote.
  HDMI
  USB 2.0
  USB 3.0
  AINA C
  KADI ya SD
  802.11ac Wi-Fi
  Yenye Kasi Sana
  ZenBook UX310 inakuwezesha kujiunganisha kwa haraka zaidi kwa kutumia 802.11ac Wi-Fi ya karibuni ambayo ina kasi zaidi ya hadi 2.8 kuliko 802.11 b / g / n! Na Bluetooth® 4.1 inakuwezesha kuunganisha vifaa vyako unavyovipenda bila kuathiri maisha ya betri yako. ZenBook UX310 inakupa uhuru wa kufanya chochote unachohitaji kufanya, popote unapotaka kufanya hivyo!
    Kasi ya 2.8 X
  802.11ac
  Kasi ya 2.8X
  802.11b / g / n
  Uingizi
  Kibodi ya Kipekee yenye Taa.
  Kibodi nzima yenye taa ya ZenBook UX310 imejengwa kwa njia ambayo inakupa mazingira mazuri ya kuandika. Inakidhi sana katika kuongeza ufanisi wa kazi, ikiwa na vitufe vya 1.6mm vinakufanya ujisikie vizuri katika matumizi. Taa zinazowaka kwa nyuma zinafanya iwe rahisi kuitumia kwenye mwanga hafifu.
    Mwachano wa 1.6 mm
  Muundo Imara Uliokatwa kwa Mkasi
  Mguso wa Ubora wa Hali ya Juu.
  Tachipadi iliyofunikwa kwa kioo inayotumia teknolojia ya vioo vya simu za kisasa ili kuwa na uwezo mzuri wa kuhisi pamoja na usahihi wa kipekee. Tachipadi inajumuisha kibaini alama za vidole cha hali ya juu, kwa ajili ya kuingia kuliko salama kwa kasi na kwa urahisi*. Na kama ilivyo ZenBook, inaonekana nzuri pia, ikiwa na mwisho uliokatwa kwa umbo la almasi kuizunguka.
  Sauti
  ASUS SonicMaster:
  Iliyoundwa Kutoa Sauti ya Kipekee.
  Daima sauti ya kipekee imekuwa kipengele cha familia ya ZenBook. Iliyoundwa kwa kushirikisha timu ya ASUS Golden Ear na Harman Kardon, teknolojia ya ASUS SonicMaster inatoa sauti ya kipekee zaidi kwenye kompyuta pakato. Mchanganyiko bora wa vifaa na programu zilizotengenezwa vizuri ili kuhakikisha ZenBook UX310 inakupa sauti ya kipekee.