ASUS recommends Windows 10 Pro for business.

  ASUS VivoBook 15 X540UA

  Rudi juu
  Muundo wa kijadi.Rangi za kuvutia
  Iliyoundwa kwa ajili ya Uzalishaji na Burudani
  Toleo la ASUS X540 linaendeshwa na processors za Intel® ili kukupa matumizi laini na sikivu ya kompyuta.Ikiwa na graphics za NVIDIA® GeForce® 900 Series zilizo bora, utawala uliowekwa tayari wa kumbukumbu, hadi 12GB RAM, na Windows 10, X540 ni jukwaa bora la kufanyia shughuli za kompyuta kila siku.
  Windows 10 Home
  Utendaji wenye nguvu sana na SSD
  Pata maboresho makubwa kwenye kasi ya usomaji au kuandika, utendaji wa PCMark,muda wa kuwaka, na ulinzi kamili wa data unapoifanya kompyuta yako ya ASUS VivoBook 15 X540 Series kuwa ya SSD.
  Sauti Inayotanuka, Iliyotuniwa na Wataalamu
  Mchanganyiko wa vifaa, programu, na kutuni, SonicMaster ilitengenezwa kwa lengo dhahiri la kukupa sauti bora ya kompyuta ya notebook.Codec mahiri huhakikisha uzalishaji kamili wa sauti; wakati amplifaya iliyoboreshwa, spika mkubwa na vyumba vya sauti hutoa sauti yenye nguvu na besi nzito.Uchakataji wa ziada wa mawimbi husaidia kuboresha utendaji wa vifaa, kuchuja kelele na kuboresha usahihi wa sauti ili uweze kufurahia sauti ya kipekee kwenye matoleo X yako.
  Muundo wa Spika Uliosanifiwa ili kutoa sauti bora
  Spika za mviringo za X540 huongeza kila milmeta za ujazo za kiuzi kilichopo ili kukupa sauti nzuri yenye mawimbi ya chini na iliyopunguzwa kelele.Vyumba vikubwa zaidi vya 19.4cc hukupa besi bora na usikivu bora wa sauti.
  Spika ya Mviringo
  420
  20Khz
  Ni rahisi kuboresha sauti kwa kutumia AudioWizard ya kipekee
  AudioWizard inakusaidia kutuni sauti yako kupitia modi tano zilizowekwa tayari.Kiolesura chake rahisi na kinachovutia hukuwezesha kuhama kutoka modi moja hadi nyingine ili upate sauti bora kwa ajili ya maudhui yoyote, kwenye mazingira yoyote.Au kama unapendelea, tawala mipangilio wewe mwenyewe.
  Modi ya mziki huzileta nyimbo zako unazozipenda kwenye maisha, huku modi ya filamu hukupa sauti yenye ubora wa sauti ya sinema.Modi ya kurekodi huboresha mipangilio ili upate sauti safi isiyokuwa na mikwaruzo unaporekodi.Modi ya michezo ya kompyuta hukuzamisha kikamilifu kwenye mchezo, wakati modi ya usemi huhakikisha majadiliano yanakuwa bora.
  Kucheza michezo ya kompyuta
  Filamu
  Muziki
  Kurekodi
  Usemi
  Kutuni AudioWizard-Iliyoboreshwa
  Ili kurekebisha mipangilio ya sauti ili iendane na kile unachopendelea, ASUS AudioWizard ina modi tano zinazochagulika.Modi ya muziki huleta nyimbo zako unazozipenda kwenye maisha, wakati Modi ya filamu inatoa uhalisia wa kweli wa sinema.Modi ya kurekodi inakupa rekodi bora zisizokuwa na mikwaruzo, na Modi ya michezo ya kompyuta inakuongezea wigo wa kufurahia michezo yako unayoipenda.Hatimaye, Modi ya usemi hufanya sauti iwe safi na yenye nguvu.
  Kucheza michezo ya kompyuta
  Filamu
  Muziki
  Kurekodi
  Usemi
  Imemaliziwa kifahari.Muundo Mwepesi
  ASUS X540 ina kiunzi imara chepesi amabacho kina uzito wa 1.9kg – bora kwa ajili ya kusafiri au unapotaka kufanya hivyo.Umaliziaji bora wa kipekee unaovutia unakufanya uonekane kwa upekee kwenye kundi.
  1.9 kg Wepesi wa Unyoya
  Furahia Ulimwengu wa Rangi
  na Teknolojia ya ASUS Mng'ao
  Ili kuhakikisha unapata picha bora sana, teknolojia ya ASUS Mng'ao ina urekebishaji wa joto la rangi ili kutoa rangi iliyojaa na kukolea.

  Ina modi onyeshi nne ambazo zinaweza kufikiwa kwa urahisi.Modi dhahiri huboresha tofauti kati ya rangi na uangavu kwa ajili ya kuperuzi picha au kutazama video na filamu, Modi inayolinda macho hupunguza viwango vya mwanga wa bluu na inafaa wakati unaposoma kwa muda mrefu.Modi ya kawaida imetuniwa kwa ajili ya kazi za kila siku; wakati Modi inayowekwa na mtumiaji ni kwa ajili ya marekebisho ya rangi ya kiwango cha juu.
  Kawaida
  Kilinda Macho
  Inayowekwa na Mtumiaji
  Dhahiri
  Linda Macho Yako kwa Kutumia Modi Inayolinda Macho ya ASUS
  Paneli nyingi za LED zinatoa mwanga wa bluu - ambao ni sababu kuu ya kuzorota kwa seli za jicho na matatizo ya retina.Modi ya ASUS ya kulinda macho kwa ufanisi inapunguza viwango vya mwanga wa bluu hadi 33% ili kufanya usomaji uwe wa raha, na kukulinda dhidi ya matatizo ya macho pamoja na magonjwa mengine.
  Kilinda Macho cha ASUS
  33 % Kiwango cha chini cha mwanga wa bluu
  Modi Inayolinda Macho
  / Zima
  Modi Inayolinda Macho
  Washa
  Muundo wa Kibodi Unaokidhi Mazingira ya Kazi
  Sasa kuandika ni kwa raha kuliko ilivyokuwa kwenye matoleo X ya kibodi kamili ya chiclet.Vitufe vilivyowekwa vyema kwa mwachano na mkao wa 1.8mm, kwa hiyo utapata mguso imara wakati wa kuandika.
  Muundo imara wenye mkato wa mkasi
  1.8 mm Mwachano
  Kiingizi kinachovutia cha ASUS Smart Gesture
  Teknolojia ya ASUS Smart Gesture hutumia uboreshaji wa muunganiko bora wa vifaa na programu ili kukupa uingizi sahihi.Kwa kutumia njia ya kisasa ya utengenezaji wa skrini ya kugusa ya simu za kisasa ilizalisha tachipadi yenye uwezo mkubwa wa kuhisi inayokuruhusu kukuza na kupunguza, au kupandisha ukurasa wa picha au tovuti kirahisi kwa kutumia vidole vyako.

  Kupandisha na Kushusha Ukurasa wa Wavuti

  Juu na Chini

  Kukuza / Kupunguza

  Mfinyo wa Vidole Viwili

  Kusukuma kwa vidole 3

  Mwonekano wa kutekeleza kazi

  Kusukuma kwa vidole 3

  Mwonekano wa kutekeleza kazi

  Kusukuma kwa vidole 3 (kulia / kushoto)

  Kubadilisha desktopu

  Mguso wa Vidole 3

  Kufungua Cortana

  Inakuwa Imepoa, Hata Baada ya Saa Nyingi za Matumizi
  Teknolojia ya ASUS IceCool inayapa matoleo X muundo wa kipekee wa ndani ambao unashughulikia maswala ya joto yasiyo sawa kwa kuzuia joto kujijenga inapokuwa kiganjani.Inafanya muegemeo wa kiganjani kuwa na joto la kati ya 28°C hadi 35°C ambalo kwa kiasi kikubwa ni chini kuliko joto la mwili.Mpangilio wa kipekee wa ndani huweka sehemu zinazozalisha joto mbali nawe, na kwa kuhusisha upoozaji wa kipekee kutoka kwenye bomba na matundu ya upoozaji, ili kuhakikisha unakuwa na matumizi yenye raha hata baada ya saa nyingi za matumizi.