ASUS recommends Windows 10 Pro for business.

  R541SA

  Rudi juu
  ASUS Mng'ao
  ASUS Tru2Life Video
  ASUS SonicMaster
  ASUS GIFTBOX
  ASUS ZenAnywhere
  Iliyojaa Kushangaza
  Kwa bidhaa zetu zote, tuna lengo rahisi: kuimarisha maisha yako ya kidigitali. Programu yetu ya kipekee inaboresha sauti, muonekano na mguso ili kukupa uzoefu wa kushangaza sana. Ifurahie!
  ASUS ina programu nyingi za kipekee ambazo zimeundwa ili kuboresha kompyuta pakato yako ya ASUS. Hizi ni pamoja na zana muhimu na huduma kwa ajili ya matumizi ya kila siku ya kompyuta yako, programu za kukuongezea kiwango cha burudani, na programu za kuongeza tija. Programu hizi zote zimeundwa ili kukupa furaha na tija katika matumizi ya kompyuta pakato yako ya ASUS. Kwa hiyo usisahau kuangalia programu ya ASUS Giftbox ili kugundua mambo ya kushangaza ambayo programu ya ASUS inaweza kukufanyia!
  ASUS Mng'ao
  Rangi Bora Zilizoboreshwa
  Picha Bora, Daima.
  Tunakuwa makini sana kuhakikisha kuwa vioo onyeshi vyetu vyote vinaonyesha kila kitu vyema na kwa usahihi kadri iwezekanavyo.
  ASUS Mng'ao ni Nini?
  Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna paneli mbili za LCD zinazoonyesha rangi sawa. Hii ni kutokana na mambo mengi ambayo hayawezi kuondolewa kabisa wakati wa utengenezaji, kama vile kemia ya kioo cha kioevu (liquid crystal - LCD), tofauti za mwanga na uvumilivu wakati wa utengenezaji. Hata hivyo, tofauti hizi zinaweza kupunguzwa kwa udhibiti makini wa ubora na kubadili vyema vipimo vya kioo onyeshi. Hiki ndicho haswa ASUS Mng'ao hufanya: kwa kurahisisha, inahakikisha paneli zetu zote za vioo onyeshi zinaonyesha rangi sawa na zinazofanana. Kwenye kiwango cha kiufundi, hutumia mchanganyiko wa marekebisho ya kiwandani (zaidi sana, marekebisho ya gamma na marekebisho ya joto la rangi) pamoja na marekebisho ya programu ili kukupa kioo onyeshi chenye rangi zenye ulinganifu na usahihi bila kujali ni bidhaa gani ya ASUS unayoitumia.
  ASUS Mng'ao ina modi nne zinazoweza kubadiliwa kwa kubofya mara moja: Modi ya Kawaida, Modi inayolinda Macho, Modi dhahiri na Modi inayowekwa na mtumiaji. Modi ya kawaida inakupa mipangilio ya kiwandani iliyoboreshwa, Modi inayolinda macho hupunguza viwango vya mwanga wa bluu ili uone vizuri, na Modi dhahiri inawezesha mipangilio ya kioo onyeshi kutoa picha katika mwonekano halisi, bila kufanya rangi kuonekana siyo halisi. Modi inayowekwa na mtumiaji hukupa utawala juu ya mipangilio ya joto la rangi, kwa hiyo unaweza kubadilisha mpangilio wa kioo onyeshi ili kukidhi matakwa yako. Kimsingi, paneli za ASUS Mng'ao zimesanidiwa kuonyesha rangi sahihi kadri iwezekanavyo ili zionyeshe vitu vyema. Lakini tunatambua kwamba wakati mwingine unaweza kuhitaji kubadilisha hii - kwa mfano kuongeza 'Wow!' kidogo kwenye picha zako au video. Kwa sababu hii, tumejumuisha modi nyingine tatu zinazochagulika - Modi Inayolinda Macho, Modi Dhahiri na Modi inayowekwa na Mtumiaji — pamoja na Modi ya Kawaida
  Modi ya Kawaida
  Mchanganyiko wa gamma thabiti na joto la rangi katika paneli zote za ASUS Mng'ao inamaanisha kwamba kwenye Modi ya kawaida, rangi huonyeshwa kwa usahihi na ulinganifu, na kwa kufanana kwa karibu na rangi halisi kadri iwezekanavyo. Modi ya kawaida ni modi ya msingi kwenye ASUS Mng'ao, lakini inaweza kubadilishwa kwa urahisi kuwa modi yoyote kati ya nyingine tatu.
  Marekebisho ya Gamma
  Ikiwa na Marekebisho ya Gamma
  Bila Marekebisho ya Gamma
  Huwezi kushangaa kujua kwamba jicho la mwanadamu hufanya kazi kwa njia tofauti kwa paneli ya LCD. Paneli ya LCD inaonyesha viwango vya mwangaza katika muendelezo wa unyoofu wa hatua sawa za kidigitali, lakini utambuzi wa jicho wa mwanga siyo wa unyoofu, unatambua tofauti ya giza kuliko mwanga. Kama utambuzi wa jicho wa mwangaza kutoka kwenye nyeusi kwenda nyeupe utawekwa kwenye chati, itafuata mchirizo unaoitwa mchirizo wa gamma. Ili kile kinachoonekana kwenye LCD kifanane na mchirizo huu - kioo onyeshi huonyesha kiwango cha mwanga kama kinavyoweza kuonekana na jicho - kile kinachoonekana kwenye kioo kinabidi kirekebishwe kwa urekebisho wa gamaa. Bila urekebisho wa gamma, kioo onyeshi kitaonyesha vivuli vya rangi vichache sana, ikizingatiwa kuwa muingiliano mzuri wa vivuli utapotea.
  Ili kurekebisha gamma, wahandisi wetu wamerekebisha mwanga wa kila kivuli cha kijivu unaoonyeshwa na paneli - kutoka rangi nyeusi halisi hadi nyeupe halisi - ili kinachoonyeshwa kifuate mchirizo wa gamma. Mchakato huu wa marekebisho ya gamma pia hurekebisha tofauti ndogo za ndani ambazo ni za asili katika paneli zote za LCD. Tunafanya marekebisho haya kwa kila kioo onyeshi cha ASUS Mng'ao ili kila paneli iwe na kiwango cha kawaida cha gamma. Mchirizo huu wenye thamani ya kimahesabu ya 2.2, ambayo ni thamani ya kawaida ya gamma inayotumiwa na programu endeshi za Windows.
  &
  Joto la Rangi
  10000K
  8000K
  6000K
  4000K
  2000K
  Marekebisho ya Gamma hushughulikia tatizo la mwitikio wa jicho wa mwanga lisilo la unyoofu, lakini halifanyi kitu kingine chochote kuhusiana na usahihi wa rangi halisi. Ili kurekebisha hili, kurekebisha joto la rangi kunahitajika. Ikiwa umewahi kutazama paneli kadhaa za LCD upande mmoja hadi upande mwingine wakati zikionyesha skrini nyeupe kamili (kwa mfano kwenye duka), huenda umeona tofauti fulani katika paneli hizo. Tunatatua tatizo hili kwa kurekebisha kivuli cha skrini nyeupe halisi kuwa kiwango cha wastani kilichorekebishwa, kwenye vioo onyeshi vyetu vyote vya ASUS Mng'ao: kiwango hiki kinaitwa joto la rangi.
  Joto la juu la rangi hufanya skrini nyeupe kabisa kuonekana bluu kidogo ('iliyopoa'), wakati joto la kiwango cha chini huonekana nyekundu ikiwa na mwonekano wa 'ujoto'. Joto la rangi hupimwa kwa kipimo cha Kelvin (K), kipimo cha joto halisi. Joto la rangi ya mwanga wa mchana huchukuliwa la kawaida na paneli zote za ASUS Mng'ao zimerekebishwa kuendana na joto hili la rangi.
  =
  ASUS Mng'ao - Modi ya kawaida
  Ikiwa na marekebisho ya Gamma pamoja na Marekebisho ya Joto la Rangi. Picha unazoona kwenye paneli za ASUS zinaonekana kwa ubora unaokaribiana na jinsi unavyoona kitu hicho hicho kwa macho yako halisi.
  Modi Inayolinda Macho
  Modi Inayolinda Macho ni modi maalum iliyoundwa ili kuweka macho yako katika hali nzuri wakati wa kutazama kompyuta kwa muda mrefu.
  Inapunguza Mwanga wa Bluu
  Kukaa sana kwenye mwanga wa bluu unaozalishwa na taa bandia za kisasa - pamoja na ule unaotolewa na vioo onyeshi vya LCD - kunadhaniwa kuathiri afya ya macho. Modi ya Kulinda Macho ya ASUS hupunguza uzalishaji wa mwanga wa bluu hadi kufikia 30% (kulingana na sifa za paneli ya LCD) kwa hiyo macho yako daima yanalindwa wakati modi ya Kulinda Macho inapotumiwa.
  Bluu kidogo, Dhahiri zaidi
  Ikiwa na Modi ya Kulinda Macho
  Bila Modi ya Kulinda Macho
  Modi ya Kulinda Macho ya ASUS ni tofauti sana na mifumo mingine ya kupunguza mwanga wa bluu. Badala ya kutumia chujio rahisi ya njano iliyowekwa kwenye picha nzima, modi ya Kulinda Macho ya ASUS inapunguza mwanga wa bluu kwa msingi wa pikseli - sawa na teknolojia tunayotumia kwenye modi dhahiri. Rangi katika pikseli moja huchambuliwa ili kuona kama kuna mwanga wowote wa bluu, na kama upo, kiwango chake hupunguzwa.
  Ikiwa hakuna bluu kwenye pikseli, pikseli inaachwa bila kubadilishwa. Kwa njia hii ya hali ya juu inamaanisha kuwa mwanga wa bluu unapunguzwa tu pale inapohitajika, na hii husababisha picha kubaki na rangi zake dhahiri, ili kutoa mwonekano halisi zaidi.
  Imepoa kwenye Macho Yako, Imechangamka katika Moyo Wako
  Kwa kupitia Teknolojia Inayolinda Macho ya ASUS, tunakuleta picha za kushangaza ili kuchangamsha moyo wako, ikiwa na mwanga wa bluu uliopungua ili zionekane vizuri kwenye macho yako ya thamani. Mwanga pungufu wa bluu, lakini ni nzuri.
  Modi Dhahiri
  Kwenye modi dhahiri, tunafanya marekebisho kwenye ukolevu wa rangi ya picha yaliyofanyiwa mahesabu kwa uangalifu ili kuzifanya picha ziweze kuonekana dhahiri na za kusisimua.
  Rangi ya Asili
  Rangi ya Marekebisho
  Kujenga Ukamilifu, Pikseli kwa Pikseli
  Tofauti na wazalishaji wengine ambao huongeza tu ukanda wa rangi kwenye picha nzima, sisi tunatafuta ukolevu stahiki kwa kila pikseli binafsi. Thamani halisi ya kila pikseli hutafutwa kuendana na tabia za kipekee za paneli husika, pamoja na matokeo ya tafiti za kisaikolojia za kubaini mrejesho wa binadamu kutokana na nguvu ya rangi. Matokeo yake ni kiwango cha jumla cha ukolevu wa rangi ambao hautaonekana bandia, lakini inaboresha rangi ili kufanya picha zionekane za kusisimua.
  Modi Inayowekwa na Mtumiaji
  Ingawa tunaweka jitihada nyingi katika kuonyesha picha bora kadri iwezekanavyo, tunatambua kwamba wakati mwingine unaweza kutaka kurekebisha joto la rangi ya kioo onyeshi kutoka kwenye mpangilio wa msingi. Kwa mfano, unapofanya kazi katika mazingira tofauti ya mwanga, au ili tu kukidhi pendeleo lako kwa ajili ya kuonyesha rangi zilizopoa au zenye ujoto.
  Kidhi unachokipenda kwa joto la rangi linalorekebika
  Katika modi Inayowekwa na Mtumiaji, unaweza kurekebisha joto larangi kukidhi matakwa yako, kwa kipimo cha -50 hadi +50, kwa kutumia kitufe telezi rahisi. Kama utaunganisha kioo onyeshi cha nje cha ASUS Mng'ao kwenye kompyuta pakato ya ASUS, ikiwa ni kwa ajili ya kurudufu kioo cha kompyuta pakato au kama kioo onyeshi cha pili, ASUS Mng'ao itajizima yenyewe moja kwa moja ili kuondoa tatizo la mwingiliano. Inafanya kazi kikamilifu wakati kioo onyeshi cha nje kinapotumiwa kupanua skrini ya kompyuta pakato.
  ASUS Tru2Life Video
  Video ya pikseli-kamilifu, daima!
  Video ya pikseli-kamilifu, daima!
  Teknolojia ya video ya ASUS Tru2Life Video hufanya video zako zionekane za kushangaza. Kwa kutumia programu bora zinazoboresha kila pikseli kwenye kila fremu ya video, utafurahia ubora mkubwa wa picha kadri iwezekanavyo — kila wakati!
  ASUS Tru2Life Video ni nini?
  ASUS Tru2Life Video ni teknolojia ya kipekee ya kuboresha video inayofanana na ile inayopatikana kwenye televisheni za ubora wa hali ya juu. Inatumia kanuni za programu bora ili kuboresha ukali na uangavu wa kila fremu ya video, ili video zionekane vyema, bora na halisi zaidi. Kila wakati kompyuta yako inapotuma fremu ya video kwenye skrini, ASUS Tru2Life Video inachambua kila pikseli moja kwenye fremu na inaboresha mwanga wake na ukali wake kwa kila pikseli. Ukali Ulioboreshwa
  Tru2Life kwa akili inaweza kuboresha kiwango cha zaidi ya milioni moja za ukali kwa kila fremu, hili hutoa picha bora iliyoboreshwa inayofanana na picha halisi.
  Uangavu Ulioboreshwa
  Kanuni maizi kwenye ASUS Tru2Life Video huchambua chati ya uangavu kwa kila pikseli ya video kwenye kila fremu, kisha kwa akili inarekebisha viwango vya uangavu na kiwango cha weusi. Hii inaweza kuboresha tofauti kati ya rangi na uangavu hadi kufikia 200%, ikionyesha sehemu zilizojificha kwenye maeneo yenye giza huku sehemu zinazong'aa zikibaki kama zilivyo!
  Matokeo ya mwisho? Yenye rangi zaidi, uhalisia zaidi, na ukali wa video wenye tofauti ya kipekee kati ya rangi na uangavu! Mara baada ya kuona ASUS Tru2Life Video ikifanya kazi, utajiuliza umeishije bila kuwa nayo!
  Video ya pikseli-kamilifu, daima!
  Teknolojia ya video ya ASUS Tru2Life Video hufanya video zako zionekane za kushangaza. Kwa kutumia programu bora zinazoboresha kila pikseli kwenye kila fremu ya video, utafurahia ubora mkubwa wa picha kadri iwezekanavyo — kila wakati!
  ASUS SonicMaster
  Ukamilifu wa Sauti
  Sauti ya Kipekee
  Zaidi.
  ASUS SonicMaster inakuletea sauti yenye nguvu ya kipekee, isiyo na mikwaruzo ambayo itagusa hisia zako kwa ujazo na uzuri wake.
  Vifaa, Vilivyokamilishwa.
  Ikiwa na spika, kwa hakika ukubwa mmoja haukidhi yote. Ili kupata sauti nzuri zaidi kutoka kwenye kifaa, tulitumia muda mwingi kuhakikisha tunatumia spika ambazo zinakidhi vyema tabia halisi ya kifaa, kuchagua kwa uangalifu kutoka kwenye machaguo yenye maumbo, ukubwa na vipimo mbalimbali.
  Mara baada ya kuchagua spika bora, timu ya ASUS Golden Ear hufanya kazi kwa karibu na timu ya kubuni bidhaa ili kuhakikisha spika zimewekwa mahali sahihi kwa ajili ya utoaji wa sauti bora sana. Uamuzi huu unapaswa kuzingatia mambo mengi magumu, kama vile vipimo vya chumba cha sauti na mwelekeo wa spika zitakapolenga.
  Programu Iliyoundwa Vizuri
  Timu ya ASUS Golden Ear ni kundi la wataalamu wa sauti wanaohusika na mfumo wa sauti kwa kila kifaa. Wakifanya kazi na kampuni za teknolojia ya sauti zinazojulikana ulimwenguni, timu ya Golden Ear hurekebisha na kuboresha vifaa vya programu za sauti kwenye kila kifaa ili kuhakikisha usikivu wa sauti unakuwa wa kusisimua, na usiosahaulika.
  Kama wewe ni mtumiaji wa kiwango cha juu, unaweza kuchukua udhibiti kamili wa mipangilio ya ICEPower® graphic equalizer na kurekebisha uwiano wa mawimbi ya sauti ili kukidhi matakwa yako. (inapatikana kwa modeli zilizochaguliwa pekee) Kwa kifaa chako kinachoendeshwa na ASUS SonicMaster, kwa chanzo chochote cha sauti. Ina modi tano rahisi zilizopo - Mziki, Filamu, Michezo ya Kompyuta, Kurekodi na Usemi - ambazo zimeundwa zikiwa na mipangilio bora kwa kila moja.
  Wizadi ya Sauti ya ASUS

  Modi ya Muziki
  Modi hii inakupa sauti halisi yenye maboresho madogo, kwa hiyo kila unachokisikia ni kile ambacho mzalishaji au msemaji halisi alikusudia ukisikie.

  Modi ya Filamu
  Kwa utazamaji mzuri wa filamu, modi hii huboresha bezi na mawimbi ya juu ili kukufanya ufaidi kikamilifu maboresho ya sauti ya filamu yenye nguvu, kama vile ukiwa kwenye sinema.

  Modi ya Michezo ya Kompyuta
  Hii ni kwa ajili ya wakati unapotaka kuboresha kila sifa ya sauti kwenye mchezo wa kompyuta: sauti ya injini kwenye michezo ya mashindano, au sauti halisi ya milipuko kwenye uwanja wa vita. Ukiwa na modi ya michezo ya kompyuta iliyoongezewa mambo kadhaa, utaweza kuufurahia ulimwengu zaidi ya udhanifu wako.

  Modi ya Kurekodi / Usemi
  Rekodi zilizogandamizwa vibaya zinawezakusikika vibaya, zikiwa na bezi mbaya na mawimbi ya juu yaliyoharibiwa. Modi ya kurekodi inahakikisha kuwa rekodi zako zote ni safi na zina uwiano mzuri.

  Modi Inayowekwa na Mtumiaji
  Kama wewe ni mtumiaji wa kiwango cha juu, unaweza kuchukua udhibiti kamili wa mipangilio ya ICEPower® graphic equalizer na kurekebisha uwiano wa mawimbi ya sauti ili kukidhi matakwa yako. (inapatikana kwa modeli zilizochaguliwa pekee)
  ASUS GIFTBOX
  Programu kubwa, Kwa ajili yako tu!
  ASUS GIFTBOX ina programu nyingi maarufu na ofa za kipekee zilizopendekezwa ili kuboresha kompyuta pakato yako ya ASUS. Hizi ni pamoja na zana muhimu na huduma kwa ajili ya matumizi ya kila siku ya kompyuta yako, programu za kukuongezea kiwango cha burudani, na programu za kuongeza tija.
  ASUS GIFTBOX ni nini?
  ASUS GIFTBOX ni lango linalokuwezesha kufikia mamia ya programu za karibuni, maarufu zaidi zilizopo, ikihusisha programu kutoka kwenye Window Store, programu za msingi za kompyuta na programu za wavuti. ASUS GIFTBOX inaonekana mara unapofungua kompyuta pakato yako mpya ya ASUS kwa mara ya kwanza, ikikupokea kwa bashasha kwenye familia ya ASUS. Inakupa uwezo wa kubinafsisha kompyuta pakato yako kwa kutumia programu unazozifahamu na kuzipenda, kwa hiyo kompyuta pakato yako mapema kabisa itaakisi wewe ni nani na unapenda nini.
  Unachokipata papo hapo
  ASUS GIFTBOX inakuwezesha kuchagua programu unazozipenda papo hapo. Mara unapowasha kompyuta pakato yako mpya ya ASUS, ASUS GIFTBOX hutokea, ikikusubiri upakue programu yoyote kati ya mamia ya programu zilizopo kwa ajili yako. Ikiwa na usanidi wa haraka na rahisi, hakuna muda unaopotea.
  Manufaa ya kipekee kwa ajili yako
  Sasa wewe ni sehemu ya familia ya ASUS, furahia punguzo kwenye programu za kulipiwa na manufaa ya ASUS ya kipekee. Hakikisha unaingia mara kwa mara ili uone ofa zetu za hivi karibuni. ASUS GIFTBOX hutoa punguzo na mikataba kwenye programu za kulipiwa, hii ni kwa watumiaji wa ASUS pekee. Ukiwa sehemu ya wachache, utafurahia punguzo la bei ya mamia ya programu maarufu zaidi zinazopatikana huko. Hakikisha unaingia mara kwa mara. Kila mara tunaongeza mikataba mipya ya kipekee ambayo itakuwezesha kuokoa pesa kwenye programu zako unazozipenda.
  Programu zote utakazozihitaji
  ASUS GIFTBOX inakupa uwezo wa kuchagua mamia ya programu za msingi za kompyuta, programu za wavuti, na programu kutoka kwenye Window Store. Tunaonyesha tu programu bora, maarufu sana tunazojua kuwa utazipenda. Programu zetu mbalimbali zinahakikisha kwamba utapata kile unachokitafuta. Ikiwa unapendelea michezo ya kawaida au programu za uzalishaji, ASUS GIFTBOX inakidhi hayo yote. Tafuta kwa kategoria, au tazama programu maarufu na zilizokubaliwa zaidi zilizopakuliwa leo.
  ASUS ZenAnywhere
  Fikia Kompyuta Yako Popote
  Fikia Kompyuta Yako Popote
  ZenAnywhere ni huduma ya kimtandao ambayo ni rahisi na salama inayokuruhusu kufikia data zako binafsi na kamera kwenye kompyuta yako ya ASUS. Pia hata kwa kupitia mtandao hukuwezesha kuiamsha kompyuta yako, kuiweka kwenye modi ya kulala au kuizima. ZenAnywhere ni rahisi kuiweka — tengeneza akaunti, ingia na utakuwa tayari kuendelea!
  Xplorer ya Faili
  ZenAnywhere ni pamoja na Xplorer ya Faili - kiolesura kinachokuruhusu kufikia na kuhifadhi nyaraka zako, picha au mafaili ya mziki na video. Inakuwezesha kuvinjari, kuhifadhi au kusoma mafaili kwenye folda lolote, ikihusisha yale yaliyohifadhiwa kwenye vifaa vya nje vya kuhifadhi data. Unaweza hata kutumia ASUS PC yako kama hazina pepe binafsi ili kupata nafasi ya ziada ya kuhifadhi data. Ufichamishi wa kiwango cha kijeshi unatoa ulinzi mkubwa hivyo utaweza kufikia na kuyapitia mafaili yako kwa usalama, mahali popote na muda wowote!
  Ufikiaji wa Kamera ya Wavutini
  Fuatilia mambo — popote ulipo — ukiwa na kipengele cha ZenAnywhvere Webcam Access Fikia kamera yako ya wavuti moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi, au wezesha kipengele cha kibaini mijongeo na kiweke kitume vitaarifu kwa wakati halisi. Ikiwa mjongeo utabainika, mfumo utarekodi video moja kwa moja na kuihifadhi, hivyo utaweza kuitazama baadaye.
  Uamshaji wa Kompyuta kwa Kupitia Mtandao
  Uamshaji wa Kompyuta kwa Kupitia Mtandao wa ZenAnywhere* unakuruhusu kuwasha kompyuta yako ukiwa popote — hatakama imezimwa!**
  Siku 365* za majaribio tu. Kulipia kujiunga kunahitajika baada ya kipindi cha majaribio.

  ** Kompyuta inahitajika kuwa imeunganishwa kwenye umeme na mtandao wa Intaneti. Baadhi ya kompyuta zinaweza kushindwa kumudu kipengele cha Uamshaji wa Kompyuta kwa Kupitia Mtandao kutokana na mapungufu ya kivifaa. Tafadhali rejea sifa za bidhaa kwa maelezo zaidi.
  Remote Desktop
  Kwa Desktop Remote * unaweza kutawala kompyuta yako ukiwa mbali mahali popote duniani!** Furahia matumizi ya Windows kwenye simu ya kisasa ya Android™ au iOS.
  Siku 15* za majaribio tu. Kulipia kujiunga kunahitajika baada ya kipindi cha majaribio.
  ** Programu ya Windows 10 Pro inahitajika kwa ajili ya Remote Desktop. Tafadhali rejea sifa za bidhaa kwa maelezo zaidi.
  Usanidi Rahisi
  Hatua ya 1: Fungua programu ya ZenAnywhere kwenye kompyuta yako ya ASUS* na ujisajili kwa akaunti.
  * Tafadhali rejea orodha ya utangamano ili kuona kama kompyuta yako ina uwezo huo.

  Hatua ya 2: Pakua programu ya ZenAnywhere kutoka kwenye Google Play ™ au App Store® na uingie kwa kutumia taarifa za akaunti yako.
  Hatua ya 3: Umekamilisha! Sasa unaweza kuivinjari kwa urahisi kompyuta yako ya ASUS kupitia simu yako ya kisasa.
  Usalama
  Ufichamishi wa kiwango cha kijeshi wa AES 256-bit unalinda data zote ili kuweka mafaili yako binafsi na nyaraka zote salama.
  Usanidi Rahisi
  Hatua ya 1: Fungua programu ya ZenAnywhere kwenye kompyuta yako ya ASUS* na ujisajili kwa akaunti.
  * Tafadhali rejea orodha ya utangamano ili kuona kama kompyuta yako ina uwezo huo.

  Hatua ya 2: Pakua programu ya ZenAnywhere kutoka kwenye Google Play ™ au App Store® na uingie kwa kutumia taarifa za akaunti yako.
  Hatua ya 3: Umekamilisha! Sasa unaweza kuivinjari kwa urahisi kompyuta yako ya ASUS kupitia simu yako ya kisasa.
  Usalama
  Ufichamishi wa kiwango cha kijeshi wa AES 256-bit unalinda data zote ili kuweka mafaili yako binafsi na nyaraka zote salama.