ASUS recommends Windows 10 Pro for business.

  ROG Strix GL703

  INATOSHELEZA KIU YAKO YA USHINDI

  ROG Strix GL703 hutoa zana zote muhimu ili kuongeza ujuzi wako wa mchezo kwenda ngazi inayofuata. Inatengenezwa na Intel mpya zaidi® Core ™ i7 processor, hadi picha za NVIDIA® GeForce® GTX 1060, na Windows 10 Pro, Strix GL703 inakuwezesha kudhibiti ushindani. Ongeza kasi, jikite, na kuwa tayari kushinda!

  Tazama video

  Yote MPYA ROG STRIX

  SANAA YA KISASA, KWENYE NYEUSI NA NYEKUNDU

  Strix GL703 mpya ina mwonekano wa kung'aa kama ilivyo kwa utendaji wake wa nguvu. Kifuniko chake chenye weusi uliosuguliwa kinaonyesha lengo la ndani na ukisasa unaomilikiwa na wachezaji mahiri — wale wanaojua kuwa watulivu hata wakati wa mapambano makali. Kinyume chake, nyekundu iliyojaa ya ujoto huwakilisha damu kwenye utafutaji wa ushindi, wakati umaliziaji wenye mbonyeo maalumu kwenye kifuniko cha Strix GL703 huifanya kuwa kitu cha kisasa.

  UTENDAJI WA HALI YA JUU

  Anza uzoefu wako wa michezo ya kompyuta kwa ulaini na Strix GL703! Kizazi cha 7 cha karibuni cha Intel Core i7 quad-core processor na NVIDIA® GeForce® GTX 1050 (iliyofanyiwa overclocked-kiwandani kwa 100MHz) au graphics za 1060 hutoa utendaji ambao ni bora kwa ufanisi wako wa michezo ya kompyuta. Strix GL703 pia inatoa hadi 32GB ya kumbukumbu ya DDR4 vyenye kasi ya 2400MHz - zaidi ya RAM ya kutosha kwa ajili ya michezo ya kompyuta huku ukistrimu video au kutumia intaneti!

  * Sifa zinaweza kutofautiana kulingana na usanidi.

  2.95kg
  Uzito
  2.4cm
  Kimo

  UCHEZAJI WA MICHEZO YA KOMPYUTA WENYE KASI KUBWA

  Strix GL703 inajulikana kwa ufanisi na utendaji bora: Yenye uzito wa 2.95kg tu, na umbo jembamba la 2.4cm, Strix GL703 inakuja na agile gaming firepower ambayo inakuwezesha kufurahia michezo ya kompyuta wakati wowote na mahali popote.

  2.95kg
  Uzito
  2.4cm
  Kimo
  Paneli ya Mwonekano-mpana
  100%
  sRGB
  50%
  Ya Kung'aa

  MIONEKANO YA KUSHANGAZA

  Strix GL703 ina paneli kubwa ya mtazamo mpana ambao inang'aa zaidi ya 50% kuliko modeli shindani, na hutoa rangi ya 100% ya rangi ya SRGB - hivyo inakidhi aina zote za michezo ya kompyuta. Strix GL703 pia inakuja na ROG GameVisual, zana rahisi kuitumia ambayo ina modi sita ambazo zinaweka mapendeleo yako kwa aina mbalimbali za michezo ya kompyuta, ikiongeza kasi na ubora wa rangi. Utafurahia picha kali, wazi na rangi sahihi na thabiti kutoka kwenye pembe zote za utazamaji — kwa uchezaji mzuri wa michezo ya kompyuta unaokuweka karibu na uhalisia!

  * Sifa zinaweza kutofautiana kulingana na usanidi.

  Paneli ya Mwonekano-mpana
  100%
  sRGB
  50%
  Ya Kung'aa

  UZOEFU HALISI WA UHALISIA ONYESHI (VR)

  Strix GL703 inajumuisha GeForce GTX 1060 GPU iliyo tayari kwa ajili ya uhalisia onyeshi (VR) ambayo inatoa uchezaji wa michezo ya kompyuta laini na usiokwama kwa ajili ya uhalisia onyeshi usiosahaulika. Weka hediseti yako tayari na anza safari yenye uhalisia kamili!

  * Sifa zinaweza kutofautiana kulingana na usanidi.

  200%
  kiasi kikubwa

  UBORA WA SAUTI ULIOBORESHWA

  TEKNOLOJIA YA SMART AMPLIFIER

  Strix GL703 inayapa masikio yako sauti ambayo hutoisahau! Teknolojia ya smart amplifier inatoa sauti yenye nguvu ya michezo ya kompyuta — hadi kiwango cha juu cha 200% — na kupunguza mvurugano ili kuhakikisha utendaji mzuri. Moja kwa moja mfumo hukagua na kupunguza nguvu ya kinachotoka ili kuzuia uharibifu unaoweza kutokana na kupata moto sana au kuzidiwa.

  200%
  kiasi kikubwa
  Tuli
  Kupumua
  Mzunguko wa Rangi
  Modi ya Kanda-Nyingi

  ING'ARISHE KWA AURA RGB

  Strix GL703 imejengewa teknolojia ya Aura RGB illumination, kwa hiyo unaweza kurekebisha mwanga ili kukidhi mtindo na hisia za uchezaji wa michezo ya kompyuta! Vitufe vipya vilivyoundwa kwa ajili ya ufikiaji rahihi wa ndani ya mchezo na kitawala mwendo: Chenye kinyamazishi, kuongeza au kupunguza sauti na batani za ROG Gaming Center ziko mahali sahihi unapozihitaji, utawala kamili uko kwenye vidole vyako. Kibodi inajumuisha kikundi muhimu cha vitufe vya WASD na teknolojia ya ant-ghosting na mtandazo wa vitufe wa n-key ili kuhakikisha kuwa unachoingiza kinachukuliwa kwa usahihi, bila kujali ni vitufe vingapi vilivyobonyezwa; na vitufe vyenye ukubwa wa 0.25mm vimeundwa kwa usahihi ili kukupa uandishi sahihi.

  Tuli
  Kupumua
  Mzunguko wa Rangi
  Modi ya Kanda-Nyingi

  RAFIKI WA MABINGWA

  SONIC STUDIO & SADIC RADAR

  Strix GL703 inajumuisha programu ya ROG Sonic Studio yenye uondoaji wa kelele kwenye mchezo na teknolojia ya uimarishaji wa sauti, ili kutoa mazungumzo na sauti inayosikika vizuri, yenye nguvu na ya kufurahisha zaidi. Sonic Radar huwasaidia wacheza michezo ya kompyuta kuwabaini wapinzani kupitia sura maalumu inayoonekana kwenye kioo ambayo inaonyesha nafasi halisi ya upigaji risasi, hatua za miguu na maboresho mengine ya ndani ya mchezo ya sauti. Kupitia Sonic Studio na Sonic Radar, wacheza michezo ya kompyuta hufurahia ubora wa juu wa sauti ya kwenye mchezo ambayo hutoa faida ya kimkakati.

  KITUO CHA KUCHEZA MICHEZO YA KOMPYUTA CHA ROG

  Kwa kutumia mbonyezo mmoja wa kitufe cha urahisisho, ROG Gaming Center inakuwezesha kuona dashibodi inayojitosheleza yenye taarifa muhimu, ikihusisha frikwensi ya CPU na GPU, volteji na joto. Unaweza kutumia paneli ya udhibiti ili kurekebisha matumizi ya nishati ya CPU na GPU kwa wakati halisi! ROG GameFirst IV, ROG Aura Core, XSplit GameCaster, NVIDIA GeForce Experience, na mipangilio ya programu ya ASUS Mng'ao inaweza kufikiwa kwa urahisi kupitia Kituo cha Michezo ya Kompyuta. Kituo cha Michezo ya Kompyuta pia kinapatikana kupitia programu ya ROG Android, kwa hiyo unaweka udhibiti wote karibu, bila kuharibu uchezaji wa mchezo.

  * Sifa zinaweza kutofautiana kulingana na usanidi.

  WEKA KATIKA HALI YA KUPOA NA ENDELEA

  Strix GL703 ina muundo wa hali ya juu ambao unatumia bomba nyingi maalumu za kukabili joto pamoja na feni mbili ili kuongeza utendaji wa CPU na GPU. Hii inakuwezesha kuendesha CPU na GPU kwa kasi kamili bila kupata matatizo ya joto, na inamaanisha utafurahia utulivu kamili wakati wa mapigano makali zaidi!

  UBORESHAJI WA HARAKA WA KUMBUKUMBU

  Kuisukuma ROG Strix GL703 zaidi inachukua tu sekunde moja! Paneli rahisi ya uboreshaji inaweza kuondolewa kwa urahisi, kukuruhusu kufurahia hazina data isiyo na shida yenye kasi kubwa!

  IMEUNDWA VIZURI KWA AJILI YA MUUNGANIKO

  Strix GL703 inatoa muunganisho kamili kwa mahitaji yako yote ya michezo ya kompyuta. Tumeweka matundu yanayotumiwa mara nyingi mahali ambapo utayafikia kwa haraka bila mwingiliano mkubwa — kwenye upande wa kushoto. Pia, matundu manne ya USB 3.1 Gen 1 yanatosha kwa ajili ya usanidi wa uhalisia onyeshi (VR), kipanya, na viendeshaji. Pamoja na HDMI 2.0 na tundu la Mini DisplayPort 1.2, la kuunganisha vifaa vya michezo ya kompyuta vya hivi karibuni pamoja na Strix GL703 ni rahisi.

  WI-FI YENYE KASI, NA MUENEO MPANA

  Strix GL703 imehandisiwa na Wi-Fi ya 867Mbps 802.11ac 2x2 yenye kasi ya wireless ambayo ni hadi kasi ya 6X kuliko 802.11n. Kupitia antena mbili zinazowezesha kustrimu data kusikokatika, kwa wakati mwingi utafurahia kipimo data chenye kasi kubwa, kwa ajili ya uchezaji wa michezo ya kompyuta na kustrimu — pamoja na kuongezeka kwa upeo wa kwenda huku au huko kuliko ilivyokuwa kabla!

  © 2017 Shirika la NVIDIA. NVIDIA, nembo ya NVIDIA, na GeForce, GTX, na NVIDIA GameWorks ni alama za kibiashara au alama za biashara zilizosajiliwa za Shirika la NVIDIA. Haki Zote Zimehifadhiwa.