Notisi ya Masharti ya Matumizi / Sera ya Faragha

  Notisi ya Masharti ya Matumizi

  BIDHAA ZOTE NA HUDUMA (“HUDUMA”) ZINAZOTOLEWA NA ASUSTEK COMPUTER INC. (“ASUS”) ZINATAWALIWA NA NOTISI HII YA MASHARTI YA MATUMIZI (“NOTISI”). HUDUMA INAMAANISHA, INAJUMUISHA LAKINI HAIJAZUILIWA KWENYE, BIDHAA YOYOTE, TOVUTI, TUKIO LA KWENYE TOVUTI (KAMA ILIVYOBAINISHWA HAPA CHINI), PROGRAMU NA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA MTUMIAJI CHINI YA CHAPA YA ASUS AU CHAPA NYINGINE INAYOMILIKIWA NA ASUS. UNATHIBITISHA KUWA UMESOMA NOTISI HII NA KUELEWA HAKI, WAJIBU NA VIGEZO NA MASHARTI YALIYOELEZWA HAPA. IKIWA WEWE NI MDOGO, NI LAZIMA UJISAJILI KAMA MWANACHAMA AU TUMIA HUDUMA MARA TU BAADA YA MZAZI WAKO (AU MLEZI) KUSOMA NA KUELEWA HAKI, WAJIBU, VIGEZO NA MASHARTI YALIYOKO KWENYE NOTISI HII. KWA KUENDELEA KUSAKINISHA, KUNAKILI, KUPAKUA, KUFIKIA, KUNUNUA, KUINGIA NA/KUTUMIA HUDUMA VINGINEVYO, WEWE AU WAZAZI WAKO (AU MLEZI) WANAKUBALI KUFUATA NOTISI HII, IKIHUSISHA TOLEO LILILOBORESHWA, NA SHERIA NA KANUNI ZOTE ZINAZOHUSIKA.

  Kukiri
  1.1
  WEWE unakubali kuwa HUDUMA hii itafanya kazi tu kwenye vifaa na programu zilizowekwa. WEWE unakiri kwamba ni wajibu WAKO kuwa na programu sahihi, vifaa na muunganisho wa mtandao ili uendelee na toleo la sasa la HUDUMA. ASUS, kwa hiari yetu pekee, tunaweza kurekebisha HUDUMA, kusitisha matukio yoyote yanayofanyika kupitia HUDUMA (“Tukio la Kwenye Tovuti”), au kusitisha huduma yoyote kwenye HUDUMA wakati wowote bila ya taarifa, na ASUS pia ina haki zote kuacha kutoa msaada kwa vifaa vyovyote au programu wakati wowote bila taarifa.
  1.2
  WEWE umekubali kuwa baadhi ya maudhui ya HUDUMA hutolewa na watu wengine, na WEWE unakubali kwamba HUDUMA hii inaweza kuwezesha upatikanaji wa huduma au tovuti za wahusika tofauti. WEWE unakubali kufurahia huduma hizo au tovuti na kuzifikia kwa hiari yako WEWE mwenyewe na raha hiyo itakuwa chini ya masharti kati yako WEWE na watu hao wengine, ikiwa ni pamoja na lakini sio tu kwa bei ya biashara, mifumo ya uthibitisho, kiasi cha kiwango cha utaratibu, uwasilishaji wa bidhaa na sera ya malipo. WEWE pia unatambua na kukubali kwamba ASUS haitawajibika kwa makubaliano kati yenu na watu hao wengine au maudhui yoyote yaliyotolewa na watu hao.
  1.3
  WEWE unakiri kwamba programu yoyote uliyopakua au kupatikana kupitia HUDUMA itatumika kwa kufuata Mkataba wa Leseni ya Mtumiaji ("EULA") iliyotolewa au iliyomo.
  1.4
  WEWE unakiri kwamba hakuna chochote katika NOTISI hii kinachokupa WEWE haki ya kutumia alama zozote za kibiashara za ASUS, alama za huduma, majina ya bidhaa au huduma, kauli mbiu, nembo au picha isipokuwa WEWE umekubaliwa kwa maandishi na ASUS.
  1.5
  WEWE unakubali kwamba NOTISI hii inaweza kutaja miongozo mengine, notisi, mikataba au vigezo na masharti mengine ya Tukio la tovuti iliyotolewa na ASUS au maelezo yoyote yaliyomo kwenye HUDUMA, na kumbukumbu hiyo itakuwa sehemu muhimu ya NOTISI hii.
  1.6
  WEWE unakubali kwamba ASUS ina haki ya kurekebisha NOTISI hii wakati wowote, na mabadiliko hayo yataanza kutumika baada ya kuwekwa kwenye HUDUMA. WEWE kuendelea kutumia HUDUMA baada ya mabadiliko hayo itatambulika kuwa WEWE umekubali kuyafuata na WEWE umeikubali NOTISI iliyorekebishwa. Kwa hiyo ni muhimu WEWE kusoma na kutembelea HUDUMA hii mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa WEWE unataarifa za karibuni kama NOTISI inavyoeleza. Ikiwa WEWE hukubaliani na NOTISI hii na kuzingatia sheria zote zinazohusika, unapaswa kuacha kutumia HUDUMA mara moja.
  1.7
  WEWE unakubali kuwa mfumo wa kielektroniki ndiyo njia pekee ya tamko rasmi la dhumuni la HUDUMA au NOTISI hii.
  1.8
  WEWE unakubali kwamba NOTISI hii inaweza kurejewa ili kulinda haki yako WEWE, WEWE unapaswa kuendana na desturi ya maombi ya kwenye mtandao wa Intaneti. WEWE unakubali kuwa matendo yafuatayo yamezuiliwa vikali:
  1.8.1
  Jaribio lolote la kuingilia, kuvamia, au kuharibu mfumo wowote au rasilimali kwenye mtandao.
  1.8.2
  Kuhamisha maudhui yanayotisha, machafu, picha za ngono, au kuharibu utaratibu na desturi za umma.
  1.8.3
  Kueneza virusi vya kompyuta kupitia mtandao wa HUDUMA.
  1.8.4
  Kutumia ukwapuaji wowote wa data, roboti, au zana nyingine za ukusanyaji au wizi wa data. Katika tukio ambalo WEWE unatumia programu yoyote au vifaa vilivyotajwa hapo juu, WEWE utakosa sifa za kushiriki kwenye Tukio la Tovuti.


  Haki Miliki ya Kiugunduzi
  2.1
  WEWE umekubali kuwajibika pekeyako kwa kupakia taarifa, kutuma, kuingiza au kutoa kwenye HUDUMA WEWE mwenyewe, na hakuna taarifa kama hiyo inawakilisha maoni ya ASUS. Kwa kuepuka shaka, habari hujumuisha bila ukomo kwenye, taarifa, data, maandishi, programu, muziki, sauti, picha, michoro, video, ujumbe au maudhui mengine (“Taarifa”).
  2.2
  WEWE unapopakia, unapohamisha, unapoingiza au kutoa Taarifa kwenye HUDUMA hii, WEWE unaipa ASUS, washirika wake na taasisi, duniani kote, haki isiyotenga, isiyopingika, ya bure, inayohamishika, inayoweza kupewa mtu mwingine ya kutangaza na kusambaza sehemu au taarifa zote katika muundo wowote wa media, zikiwa zimebadilishwa au laa, kuzalishwa upya, utangazwaji wa umma, usafirishwaji wa umma, kumilikishwa, kusambazwa, kuchapisha, kutolewa kwa umma, au kutumiwa kwa matumizi mengine.
  2.3
  Ikiwa WEWE huna idhini ya haki hapo juu, tafadhali usipakie, usitumie, kuingiza au kutoa Habari kwenye HUDUMA hii.
  2.4
  Ikiwa unashutumiwa kuwa umevunja haki yoyote ya watu wenine (IPR) kwa mara tatu au zaidi, ASUS ina haki ya kusitisha na / au kuzuia ufikiaji wako kwenye HUDUMA.
  2.5
  Vitambulisho na haki miliki za kiugunduzi ndani na kwa maudhui yoyote ya watu wengine yaliyomo kwenye HUDUMA au yanayoweza kupatikana kupitia matumizi ya HUDUMA, ni mali ya wamiliki wa maudhui husika na yanaweza kulindwa na sheria zinazohusiana na mali na mikataba.
  2.6
  Ikiwa unatambua ukiukwaji wowote au unaotarajiwa wa maudhui yoyote ya HUDUMA, au taarifa ya ukiukwaji inahitajika kwa mujibu wa sheria husika au kanuni, tafadhali wasilisha taarifa kwa Idara ya Utekelezaji wa Kisheria ya ASUS kwa kupitia taarifa za mawasiliano zinazoonyeshwa katika NOTISI hii, ASUS itaendelea na utaratibu unaostahili kwa mujibu wa sheria zinazohusika.
  2.7
  Baada ya kupokea taarifa ya ukiukaji kutoka kwa mmiliki wa hakimiliki au wakala wake, ASUS itaondoa, kuzuia ufikiaji wako WEWE au inaweza kuchukua hatua nyingine kwa madai ya kukiuka maudhui au huduma kwa mujibu wa sheria zinazohusika. Ikiwa unaamini kwamba maudhui au huduma hizo hazikuvunjwa, WEWE unaweza kuwasilisha taarifa ya kuzuia kwa Idara ya Utekelezaji wa Kisheria ya ASUS, kwa kupitia taarifa za mawasiliano zinazoonyeshwa katika NOTISI hii, ASUS itaendelea na utaratibu unaoendana kwa mujibu wa sheria zinazohusika.


  Usajili
  Ili kutumia huduma zote zinazotolewa katika HUDUMA hii, unatambua na kukubali kufuata:
  3.1.
  WEWE unapaswa kutoa maelezo ya kweli, sahihi, ya karibuni na kamili kuhusu WEWE mwenyewe kama utaulizwa na kuombwa kwenye mchakato wa usajili wa Akaunti ya ASUS. WEWE unaweza kufikia na kusahihisha maelezo yako ya binafsi kupitia HUDUMA hii wakati wowote.
  3.2
  WEWE unaweza kuona na kubadilisha maelezo yako ya usajili kwa kuingia na kuhariri mipangilio ya akaunti YAKO kwenye HUDUMA. Kwa usalama wa akaunti YAKO, utahitajika kuingia na ID yako ya kuingia pamoja na nywila. WEWE pekee unawajibika kikamilifu kwa kulinda usiri wa nywila na jina LAKO la mtumiaji na kwa shughuli yoyote inayofanyika kwenye akaunti YAKO.
  3.3
  Ikiwa ASUS itabaini kuwa akaunti / nywila ya Akaunti ya ASUS imepotoshwa, ASUS inaweza kusimamisha au kuondoa nywila ya Akaunti ya ASUS, akaunti (au sehemu yake yoyote) au matumizi ya HUDUMA hii, na kuondoa taarifa zote zinazohusiana na Akaunti hiyo ya ASUS kwenye HUDUMA hii.
  3.4
  WEWE unapaswa kufuata NOTISI hii na hutakiwi kukiuka sheria na kanuni yoyote inayohusika. ASUS ina haki ya kuthibitisha uhalali wa uwanachama WAKO wakati wowote wakati au baada ya Tukio la tovuti yoyote, na ina haki ya kukuondoa WEWE (hata Mshindi) kutoka kwenye Tukio lolote la tovuti ikiwa ni pamoja na kukunyima sifa ya kupata tuzo YAKO ambayo inahusisha uovu wowote wa kujaribu kuvuruga au kuingilia Tukio la Tovuti bila taarifa yoyote. Kushindwa kwa ASUS kusimamia haki zake zilizoelezwa hapa haimaanishi kuwa haki hizo zimeondolewa.


  Sera ya Faragha

  Kutokana na kuheshimu taarifa binafsi, ASUS imejizatiti kulinda na kuheshimu faragha YAKO kupitia Sera ya Faragha ya ASUS.

  Leseni na Kizuio
  5.1
  Kwa mujibu wa masharti ya NOTISI hii, ASUS inakupa leseni yenye ukomo, ya kibinafsi, isiyo ya kibiashara, isiyo tenga, isyo gawika, isiyo pewa mtu mwingine, ya bila malipo ya kufikia au kuingia kwenye HUDUMA zake. Isipokuwa kwa haki zilizopatikana wazi hapa, WEWE unakubali kuwa haki nyingine zote zinabaki kwa ASUS. Haki yoyote, zikijumuisha bila ukomo, katika HUDUMA, zitabakia kuwa mali ya kipekee ya ASUS na/au wanaoipa leseni. Hakuna chochote katika NOTISI hii kinakusudia kuhamisha haki zozote hizo, au kukuvika haki hizo WEWE.
  5.2
  Hakuna Uondoaji wa Notisi: WEWE unakubali kwamba hutaondoa, halifu, kuondoa uhalali au kubadilisha notisi yoyote au dalili za haki yoyote na / au haki na umiliki wa ASUS zilizoelezwa hapa, bila kujali ikiwa notisi au kiashiria kimewekwa, kimeunganishwa kwa namna yoyote na kifaa chochote.


  Biashara-Mtandao

  Ununuzi wowote wa bidhaa na huduma / vifurushi vya msaada vinavyotolewa na ASUS, utaongozwa na masharti na sheria za duka la biashara-mtandao, tafadhali rejea mikataba ya mauzo ya ASUS na sera husika.

  Muda na Usitishaji
  7.1
  Ikiwa kwa sababu yoyote HUDUMA hii haiwezi kuendeshwa kama ilivyopangwa, ikiwa ni pamoja na lakini pasipo ukomo kwenye maswala yasiyoepukika, matatizo ya kiufundi, uingiliaji usioidhinishwa, udanganyifu au sababu nyingine yoyote iliyo juu ya uwezo wa ASUS ambayo imeharibu au kuathiri utawala, usalama, haki, uadilifu au mwenendo sahihi wa HUDUMA hii, ASUS ina haki kwa hiari yake pekee yake ya kufuta, kusitisha, kurekebisha au kusimamisha HUDUMA kutokana na maagizo yoyote yaliyoandikwa kutoka kwenye mamlaka stahiki ya serikali husika.
  7.1
  NOTISI hii itafanya kazi hadi hapo itakapositishwa na WEWE au ASUS. Haki ZAKO za kutumia HUDUMA zitasimamishwa moja kwa moja bila taarifa kama WEWE utashindwa kuzingatia sheria na masharti yaliyotajwa kwenye NOTISI hii. Katika suala hili, ASUS haitachukua jukumu lolote juu YAKO. Baada ya kusitisha NOTISI hii, WEWE utaacha kabisa matumizi yote ya HUDUMA na nakala zake, kwa ujumla au kwa sehemu.


  Kanusho la Udhamini na Ukomo wa Dhima
  8.1
  ASUS inahakikisha kuwa mfumo wa kompyuta uliotumiwa kwenye HUDUMA una kiwango cha usalama kinachostahili.
  8.2
  WEWE UNAKUBALI KUWA KIWANGO CHA HUDUMA KIMETOLEWA “KAMA KILIVYO.” HATARI YOYOTE YA UBORA NA UTENDAJI INAKUHUSU WEWE, IKIHUSISHA LAKINI BILA UKOMO KWENYE GHARAMA ZOTE ZINAZOHITAJIKA ZA MATENGENEZO NA HUDUMA. KADRI INAVYORUHUSIWA KISHERIA, ASUS HAIWEKI DHAMANA, MOJA KWA MOJA AU ILIYODOKEZWA, KUHUSIANA NA HUDUMA HII AU TAARIFA NYINGINE YOYOTE AU NYARAKA ZINAZOTOLEWA CHINI YA ILANI HII AU KWA AJILI YA HUDUMA HII, IKIWA NI PAMOJA NA LAKINI BILA KUZUILIWA KWENYE HAKIKISHO LOLOTE LA BIASHARA AU UTENDAJI KAMILI KWA AJILI YA LENGO FULANI AU DHIDI YA UKIUKAJI, AU HAKIKISHO LOLOTE LINALOTOKA NJE YA MATUMIZI AU NAMNA YA UTENDAJI. ASUS PIA HUCHUKULIA KUWA HAKUNA UDHAMINI KUTOKANA NA MATOKEO AMBAYO YANAWEZA KUPATIKANA KUTOKANA NA MATUMIZI YA HUDUMA HII AU KAMA USAHIHI AU KUAMINIKA KWA TAARIFA YOYOTE ILIYOPATIKANA KUPITIA HUDUMA HII. MAMLAKA NYINGINE HAZIRUHUSU KUONDOLEWA KWA DHAMANA FULANI AU UKOMO AU KUONDOLEWA KWA UWAJIBIKAJI KWA AJILI YA HASARA FULANI. MATOKEO YAKE, BAADHI YA MAKATAZO NA VIZUIZI VYA HAPA JUU HUENDA VISITUMIKE KWAKO.
  8.3
  HATARI YOYOTE INAYOWEZA KUTOKEA KUTOKANA NA MATUMIZI NA/AU UTENDAJI WA HUDUMA HII ITAKUWA JUU YAKO. HAKUNA TUKIO LOLOTE AMBALO ASUS, AU WANAOIPA LESENI AU MAAFISA WAKE HUSIKA, WAKURUGENZI, WAFANYAKAZI, MAWAKALA AU WASHIRIKA WATAWAJIBIKA KWA UHARIBIFU WOWOTE WA, BAHATI MBAYA, MOJA KWA MOJA, USIO WA MOJA KWA MOJA, MAALUM, WA KUADHIBIWA, AU UHARIBIFU MWINGINE WOWOTE (IKIWA NI PAMOJA NA, BILA UKOMO, FIDIA KWAUPOTEVU WA FAIDA, USUMBUFU, KUPOTEA KWA TAARIFA, AU HASARA NYINGINE YA KIFEDHA) ITAKAYOTOKANA NA AU KUHUSIANA NA NOTISI HII AU MATUMIZI YA AU KUTOKUWA NA UWEZO WA KUTUMIA HUDUMA AU SEHEMU YAKE YOYOTE, HATA KAMA ASUS ITAKUWA IMESHAURIWA KUHUSU UWEZEKANO WA HASARA HIYO. MAMLAKA NYINGINE HAZIRUHUSU KUONDOLEWA KWA DHAMANA FULANI AU UKOMO AU KUONDOLEWA KWA UWAJIBIKAJI KWA AJILI YA HASARA FULANI. MATOKEO YAKE, BAADHI YA MAKATAZO NA VIZUIZI VYA HAPA JUU HUENDA VISITUMIKE KWAKO.
  8.4
  ASUS haitawajibika kutokana na taarifa yoyote isiyo sahihi, inayosababishwa na mtumiaji wa mtandao au kwa vifaa vyovyote au programu zinazohusiana na au kutumika katika HUDUMA hii, au kwa dosari yoyote ya kiufundi, au mjumuisho wowote ambao unaweza kutokea wakati wa usimamizi wa HUDUMA hii ikiwa ni pamoja na upungufu wowote, usumbufu, kufuta, kasoro, kuchelewa kwa uendeshaji au usafirishaji, njia ya mawasiliano au simu, matatizo ya mtandao wa simu au satellite, matatizo ya kiufundi au msongamano wa trafiki kwenye mtandao au HUDUMA, matatizo ya programu, wizi au uharibifu au ufikiaji usioidhinishwa au kubadilisha viingizi na majeraha au uharibifu wowote wa kompyuta yako unaohusiana na au kutokana na kushiriki au kupakua maudhui yoyote katika HUDUMA hii.
  8.5
  Katika tukio ambalo tuzo yoyote inatolewa kwenye Tukio la tovuti, WEWE unakubali yafuatayo:
  8.5.1
  ASUS haikubali jukumu lolote la matokeo ya kodi ambayo yanaweza kutokea kutokana na kukubalika kwa tuzo YAKO. Unapaswa kutafuta mshauri binafsi wa kifedha akusaidie WEWE.
  8.5.2
  Tuzo, nzima au sehemu, hairuhusiwi kuhamishwa au kubadilishana na haiwezi kufutwa isipokuwa imeeelezwa vinginevyo.
  8.5.3
  Katika tukio ambalo tuzo haipo licha ya jitihada za busara za ASUS ili kupata tuzo, ASUS ina haki ya kuingiza tuzo mbadala ya thamani ya kiwango kidogo kilichopendekezwa, kulingana na maagizo yoyote yaliyoandikwa kutoka kwenye mamlaka ya serikali husika.
  8.5.4
  ASUS haikubali jukumu lolote kutokana na tofauti yoyote inayokuja baadaye ya thamani ya tuzo.
  8.5.5
  Katika tukio ambalo mshindi ameshindwa kuchukua tuzo ndani ya kipindi fulani cha muda unaoonyeshwa kwenye Tukio la tovuti itachukuliwa kuwa ni kupoteza haki ya tuzo, na ASUS, kwa hiari yake pekee, ina haki ya kuamua njia mbadala ya mshindi wa tuzo hiyo.


  Fidia

  WEWE unakubali kutetea, kulipa fidia na kutokuidai ASUS na washirika wake, watoa huduma, wasimamizi, wasambazaji, watoa leseni, maafisa, wakurugenzi na wafanyakazi, kutokana na hasara yoyote, madhara, madeni, na gharama kutokana na madai yoyote au mahitaji (ikiwa ni pamoja na ada za wanasheria na gharama za mahakama), kwa sababu au kuhusiana na ukiukwaji WAKO wa Notisi hii au sheria yoyote au kanuni husika, au haki ya watu wengine tofauti.

  Kwa habari zaidi kuhusu NOTISI hii na miongozo iliyorejelewa, wasiliana na Idara ya Utekelezaji wa Kisheria ya ASUS kwa barua pepe iliyosajiliwa, facsimile, barua pepe au simu kupitia:

  ASUSTeK Computer Inc.
  Mwakilishi wa Kampuni: Ndug. Jonney Shih
  Legal Affairs Center
  Legal Compliance Department
  Address: 15, Li-Te Rd., Taipei 112, Taiwan
  Email: LegalCompliance@asus.com
  Telephone: (886) 2 2894 3447
  Fax: (886) 2 2890 7674
  Iliboreshwa Machi 4, 2015 by ASUS Legal Affairs Center