ASUS recommends Windows 10 Pro for business.

  ASUS FX553VD

  NGUVU NA MTINDO
  UNAPOKUWA NA KAZI NYINGI

  ASUS FX553 ina processor ya hivi karibuni ya kizazi cha 7 ya Intel®, Windows 10, na picha za NVIDIA® GeForce® GTX 1050 katika muundo thabiti na mwepesi. ASUS FX553 inawawezesha watumiaji wake kufanya kazi kwa ufanisi popote pale.

  Utendaji wa Hali ya Juu

  ASUS FX553 inatoa utendaji wa juu unaowezeshwa na processor ya kizazi cha 7 ya Intel® Core ™ i7 pamoja na picha bora za NVIDIA® GeForce® GTX 1050 inayofanya kazi kikamilifu na DirectX® 12 ya Microsoft®. Vifaa vinakupa utendaji mzuri na wenye nguvu pamoja na muundo maridadi, mwembamba na wa kuvutia kwa ajili ya kuongeza tija kwenye ufanyaji wa kazi nyingi kwa pamoja.

  2.5mm
  Mwachano
  30
  (N-) Mtandazo wa batani
  Imetenganishwa
  Vitufe vya Mishale

  TAWALA KILA KITU

  ASUS FX553 ina kibodi iliyotengenezwa vizuri yenye taa na vitufe vya scissor-switch vyenye mwachano wa 2.5mm kwa ajili ya mibonyezo sahihi. Ina vitufe vya WASD vilivyobainishwa, kitufe kikubwa cha nafasi na vitufe vya mishale vilivyotengwa kwa ajili ya utawala sahihi na uingizi wakati wa michezo ya kompyuta.

  2.5mm
  Mwachano
  30
  (N-) Mtandazo wa batani
  Imetenganishwa
  Vitufe vya Mishale

  USANIFU MAHIRI WA JOTO

  ASUS Cooling Overboost inakuwezesha kurekebisha kasi ya feni, na ina muundo wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa ufanisi mkubwa wa upoozaji ili kuipa ASUS FX553 utulivu unaohitajika kwa ajili ya mazingira yoyote ya kazi.

  Mwonekano mpana
  Pembe
  FHD
  Mwonekano
  Isiyong'aa
  Paneli

  MIONEKANO INAYOVUTIA SANA

  ASUS FX553 ina paneli ya HD Kamili ya 15.6-inchi yenye mwonekano mpana. Paneli hii inahakikisha inakupa ulinganifu wa uangavu na rangi, hakuna badiliko la rangi hata kama unatazama ukiwa kwenye mkao mbaya. Ina umaliziaji usiong'aa pia, kwa hiyo hakuna muakisi unaowaka kukuvuruga unapocheza michezo ya kompyuta.

  Mwonekano mpana
  Pembe
  FHD
  Mwonekano
  Isiyong'aa
  Paneli

  HADI 32GB ZA DDR4

  ROG Strix GL753 inakuja na DDR4 ya 32GB ya kiwango cha wastani ili kukupa kasi kubwa, kuongeza nafasi ya hifadhi data, na ufanisi wa ajabu wa nishati.

  TUNDU LA USB AINA-C

  Tundu la USB Aina-C inayoweza kupinduliwa inakuwezesha kuunganisha vifaa vyako kwa urahisi na kasi kubwa ya kuhamisha data.

  Chuja Kelele Zote Zisizohitajika

  Vipazasauti vya safu vilivyoundwa kwa ajili ya kuchuja kelele zote zisizohitajika, hii inamaanisha kuwa ikiwa unawasiliana kwenye mazingira yenye kelele, bado sauti yako itasikika vyema.

  SAUTI IMEWEKWA NA ICEPOWER®

  Zikiwa na muundo mzuri, spika zilizojengewa zimewekwa kwa namna ambayo zinakupa usikivu mzuri sana wa sauti.