ASUS recommends Windows 10 Pro for business.

  R541SA

  ASUS VivoBook

  Sauti ya asili. Utendaji wa Nguvu.

  Kompyuta za ASUS VivoBook Max Series zimeundwa kukupa uzoefu halisi wa picha video na sauti. Inaendeshwa na processor ya hadi Kizazi cha 7 ya Intel® Core ™, picha za kiwango cha michezo ya kompyuta za NVIDIA® GeForce®, na sauti ya kipekee ya SonicMaster inayojumuisha teknolojia ya ICEpower®, matoleo ya VivoBook Max Series yanakupa picha na video bora za kipekee ambazo hazijawahi kupatikana kwenye kompyuta pakato.

  Muundo

  Rangi za kuvutia. Umaliziaji wa kushangaza.

  Imeundwa kwa ajili ya shughuli za kompyuta za kila siku, matoleo ya ASUS VivoBook Max inakuja katika rangi nyingi za kuvutia pamoja na umaliziaji mzuri unaohakikisha kuwa unakufanya kuwa bora kuliko wengine. Matoleo ya kompyuta pakato za ASUS vivoBook Max zinapatikana katika rangi za Fedha, Kahawia ya Chocolate, Bluu bahari, Nyeupe, na Nyekundu; na huonyesha ufahari, na zina umaliziaji mzuri wa chuma kilichosuguliwa vyema.

  X541
  1.9kg
  nyepesi-sana
  X441
  1.8kg
  nyepesi-sana
  14
  X441
  15”
  X541

  Picha Video na Sauti

  Iliyoundwa kwa ajili ya burudani halisi

  Kompyuta za matoleo ya ASUS VivoBook Max zimeundwa ili kukupa uzoefu halisi wa picha video na sauti. Teknolojia za kipekee za ASUS kama vile SonicMaster audio, ikihusisha teknolojia ya ICEpower®, ASUS Mng'ao, na ASUS Tru2Life Video inafanya filamu zako na muziki kuwa halisi.

  SonicMaster

  Sauti ya kustaajabisha ya ASUS SonicMaster

  ASUS SonicMaster audio, ikiwa pamoja na teknolojia ya ICEpower®, huyapa matoleo ya kompyuta pakato za ASUS VivoBook Max utoaji wa sauti usiokuwa na mikwaruzo. Matoleo ya kompyuta pakato za VivoBook Max hujumuisha spika za 3W zenye chumba cha sauti cha 24cc, na muundo hamishaji maalumu unaokupa besi nzito na sauti za kipekee. Zaidi ya hayo zimewekwa vizuri ili kukupa sauti safi yenye uhalisia wa mazingira halisi.

  3W
  spika
  24CC
  chumba cha sauti
  spika hamishi

  Wizadi ya Sauti

  Kutuni AudioWizard-kulikoboreshwa

  ASUS AudioWizard inakupa modi tano za sauti (Muziki, Filamu, Michezo ya Kompyuta, Usemi, na Kurekodi) ili uweze kupata mipangilio bora kwa chochote unachofanya. Unaweza kubadili kwa urahisi kati ya modi moja hadi nyingine kupitia kiolesura rahisi cha AudioWizard.

  Jifunze zaidi Kuhusu ASUS SonicMaster
  Muziki
  Filamu
  Kurekodi
  Mchezo
  Usemi
  Sauti halisi Sauti yenye mawimbi madogo Sauti ya piano yenye mawimbi makubwa Uboreshaji wa sifa za wimbo Maboresho ya kimichezo sauti yenye mwangwi

  Tru2Life Video

  Video ya pikseli-kamilifu, daima!

  Teknolojia ya video ya ASUS Tru2Life Video hufanya video zako zionekane za kushangaza. Kitaalamu inaboresha kila pikseli kwenye kila fremu ya video ili kuongeza ukali na uangavu wake kwa 150%, kwa hiyo utafurahia ubora mkubwa wa picha kadri iwezekanavyo — kila wakati!

  Jifunze zaidi kuhusu Tru2Life >
  150%
  ya kuimarisha uangavu
  ASUS Tru2Life

  Kilinda Macho

  Linda Macho Yako kwa Kutumia Modi Inayolinda Macho ya ASUS

  Paneli nyingi za LED zinatoa mwanga wa bluu - ambao ni sababu kuu ya kuzorota kwa seli za jicho na matatizo ya retina. Modi ya ASUS ya kulinda macho kwa ufanisi inapunguza viwango vya mwanga wa bluu hadi 33% ili kufanya usomaji uwe wa raha, na kukulinda dhidi ya matatizo ya macho pamoja na magonjwa mengine.

  Pata maelezo zaidi kuhusu ASUS Mng'ao
  Modi Inayolinda Macho
  Modi ya Kawaida
  Modi Dhahiri
  Modi Inayowekwa na Mtumiaji

  Utendaji

  Utendaji wa uhakika

  Matoleo ya kompyuta pakato za ASUS VivoBook Max zinatumia hadi processor za kizazi cha 7 za Intel® Core ™ i7 zikiwa na hadi 8GB RAM (hupanuka hadi 16GB), na picha za NVIDIA® GeForce® GT 920. Matoleo X yanakuja yakiwa na Windows 10 Home, hivyo iko tayari kwa ajili ya kazi zako zote za kila siku za kompyuta na burudani. Kwa kihifadhi data, unaweza kuchagua hard disk ya 2TB, au kuboresha solid-state drive (SSD) kwa ajili ya ufikiaji data wa haraka.

  Intel Core
  i7
  CPU
  Windows 10 Home
  OS
  NVIDIA
  920MX
  CPU

  SSD

  Utendaji wenye nguvu sana na SSD

  Pata maboresho makubwa kwenye kasi ya usomaji au kuandika, utendaji wa PCMark, muda wa kuwaka, na ulinzi kamili wa data unapoifanya kompyuta pakato yako ya matoleo ya ASUS VivoBook Max kuwa ya SSD.

  kasi ya kompyuta pakato
  5X
  haraka zaidi

  Tundu la IO

  Kuunganisha kwa haraka na kwa kasi kwa kutumia USB Aina-C

  Matoleo ya kompyuta pakato za ASUS vivoBook Max yanakupa chaguzi mbalimbali za njia za uunganishaji ambazo zinajumuisha USB 3.0 Aina C, matundu ya HDMI na VGA, 3-kwenye-1 Kisoma kadi za SD / SDHC / SDXC, na zaidi ya hayo ili kuhakikisha kuna utangamano na vifaa mbalimbali vya ziada. Tundu la USB Aina-C linalopindulika linahakikisha kuwa kuna muunganiko sahihi kila wakati, upande wa kulia juu, au juu chini. Pia hutoa kasi ya uhamishaji wa data hadi 5Gbps - karibu mara zaidi 10 ya USB 2.0. Sasa unaweza kuhamisha picha, muziki, na hata mafaili makubwa ya video kwa muda mfupi - kuhamisha filamu yenye ukubwa wa faili wa 2GB kutachukua muda wa chini ya sekunde mbili.

  hadi
  5Gbps
  ya kasi

  Uingizi

  Uingizi rahisi

  Matoleo ya kompyuta pakato za ASUS VivoBook VivoBook Max zinatumia teknolojia ya kisasa ya kibodi na tachipadi. Furahia mibonyezo mizuri na sahihi ya vitufe yenye teknolojia ya kukataa kiganja kwa ajili ya kukupa uingizi mzuri.

  Uingizi

  Jisikie vizuri unapoandika

  Kibodi ya kipimo kamili ya chiclet hukufanya uandike kwa uhuru. Imeboreshwa muundo wake wa nyuma ili kukupa muachano wa vitufe wa 2.3mm na mweleo wa wastani wa vitufe ili kukupa mibonyezo ya vitufe ambayo ni imara na sikivu.

  2.3mm
  mwachano

  Uingizi

  Tachipadi kubwa na maizi

  Tachipadi kubwa za 106mm x 74mm zinazopatikana kwenye matoleo ya VivoBook Max zina teknolojia ya kukataa viganja inayotofautisha kidole halisi na kiganja ili kuzuia kielekezi cha kipanya kujongea kusiko kwa hiari.

  11%
  kubwa zaidi

  Maisha ya Betri

  Betri inayodumu muda mrefu ya SuperBatt

  Matoleo ya kompyuta pakato za ASUS VivoBook Max yana SuperBatt betri ambayo inakupa hadi mizunguko 700 ya kuchaji - mara 3 zaidi ya maisha ya betri za kawaida.

  3X
  maisha marefu zaidi
  100% 70% 700 ya mizunguko ya kuchaji. 300 mizunguko ya kuchaji. 0 mizunguko ya kuchaji. Betri ya kawaida SuperBatt betri
  kwenye ASUS VivoBook Max