Kuhusu ASUS

    Utangulizi


    ASUS ni kampuni ya Taiwan, ya kimataifa ya kuzalisha kompyuta na vifaa mbalimbali vya kielektroniki iliyoanzishwa mnamo mwaka 1989. Ikiwa na lengo la kutengeneza bidhaa kwa ajili ya maisha maizi ya leo na kesho, ASUS ni kampuni ya kwanza duniani katika utengenezaji wa motherboard na vifaa vya michezo ya kompyuta na ya tatu kati ya wauzaji wa juu wa kompyuta za notebook.

    ASUS ilijulikana sana Amerika ya Kaskazini wakati ilipoleta mapinduzi kwenye sekta ya kompyuta (PC) mwaka 2007 kwa kupitia Eee PC ™ yake. Leo, kampuni hii inaongoza kwenye mwenendo mpya wa simu kupitia matoleo ya ASUS ZenFone ™, na inaendelea kuendeleza bidhaa za uhalisia onyeshi (virtual rality na augmented reality) pamoja na vifaa vya IOT na teknolojia ya robotiki. Hivi karibuni, ASUS ilianzisha Zenbo, roboti maizi ya nyumbani iliyoundwa kutoa msaada, burudani, na ushirika kwa familia.

    Mwaka 2015 na 2016, gazeti la Fortune liliitambua ASUS kama mojawapo ya Makampuni Mengi Yanayokubalika Sana Duniani, na kwa miaka minne iliyopita Interbrand imeiweka ASUS ya Taiwan kuwa kampuni yenye thamani sana ya kimataifa. Kampuni hii ina wafanyakazi zaidi ya 17,000, ikiwa ni pamoja na timu bora duniani ya R & D. Ikiendeshwa kwa uvumbuzi na kujikita kwenye ubora, ASUS ilipata tuzo 4,385 na ilipata mapato yanayokadiriwa kuwa dola bilioni 13.3 kwa mwaka 2016.