Kuhusu ASUS

    Notebooks za ASUS zimejaribiwa kwenye mazingira magumu sana na maeneo mageni zaidi. Baadhi ya mafanikio haya ya kipekee yamepata hadhi kubwa. Hapa tunafafanua mafanikio ambayo yameacha alama isiyofutika kwenye historia.

    Kasoro sifuri kwenye mvuto sifuri

    R & K, msambazaji mkubwa wa kompyuta na vifaa vya kielektroniki kwa ajili ya safari za anga za juu, waliwapa wana anga za juu MIR Space Station yenye notebook mbili za ASUS. Notebook zote mbili zilifanya kazi bila tatizo kwa kipindi chote cha siku 600 kwenye anga za juu.

    "Notebooks za ASUS haizipati moto kwa kupitiliza kama ilivyo kwa zile zilizotengenezwa na makampuni mengine," alisema mwana anga wa Kirusi Sergei Avdeev. “Mzunguko wa joto katika anga za juu na duniani ni tofauti kabisa. Notebook zenye mfumo mzuri wa kukabili joto pekee ndiyo zinaweza kumudu utendajikazi wa kila siku. Tulikuwa tunawasha notebook asubuhi na kuziacha siku nzima bila shida. ”

    Kuokoa maisha kutoka hewani

    NRMA CareFlight, kitengo cha huduma ya dharura ya afya na cha helikopta ya uokoaji kinachofanya kazi huko New South Wales, Australia, hutumia notebook za ASUS katika sekta mbalimbali za huduma zake. Notebook za ASUS zina jukumu muhimu katika mpango wa CareFlight yenye lengo la kuongeza viwango vya kuokoa maisha kwa waathirika wa ajali wanaosumbuliwa na majeraha makubwa ya kichwa. Matumizi ya kompyuta yanayobebeka ya notebook hizi huwawezesha CareFlight kuifikisha timu ya matibabu kwenye eneo la tukio kwa haraka zaidi kuliko gari la wagonjwa la eneo husika, na inaweza kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na majeraha ya kichwa kwa 33%.

    "Marubani wetu wote wamevutiwa sana na kompyuta pakato za ASUS M5 na wanashangazwa kwa uwezo wake wa kuhimili mitetemo ya ndege, alisema Meneja wa Mahusiano ya Jamii ya CareFlight Mark Lees. “Sasa tuko tayari kufunga kompyuta pakato za ASUS M5 kwenye ndege zetu zote na kuziunganisha kwenye kompyuta ongozi za ndani ya ndege."

    Kumudu matuta na miruko kwenye mashindano ya barabara mbaya

    Notebook za ASUS ziliwekwa kwenye kiwango kikubwa sana cha joto wakati wa mbio za PATAGONIA 2000, ambayo ilipita kati ya majangwa yenye joto kali na milima iliyofunikwa kwa theluji. Ilifanya kazi kama vifaa vya uongozaji, notebook za ASUS zilifanya kazi vyema kwa kutegemea uwezo wake wa ndani wa GPS na uwezo wa kuonyesha ramani zinazobadilika. Pia zilitumika kama zana za mawasiliano, kutoa huduma za barua pepe na video za uelekeo wa pande mbili. “Bila shaka, kompyuta za ASUS zilimudu mazingira na changamoto za safari hii vyema, bila tatizo lolote,” alisema mratibu wa mbio hizo Aviv Shweky.

    Kileleni mwa ulimwengu

    Orodha ya notebook za ASUS, ambayo inajumuisha U5, S6 (matoleo yote ya leather na bamboo), W7 na U1 zilichaguliwa na timu ya wapanda milima kwenye safari ya Mlima Everest.

    Kwenye kambi ya chini ya mlima kwenye mwinuko wa 5,000m juu ya usawa wa bahari, notebook nyingine hazikuwaka kwa sababu ya joto kuwa chini sana; lakini notebook za ASUS ziliendelea kufanya kazi. Kwa kuthibitisha teknolojia rafiki kwa mazingira, kiongozi wa timu ya msafara Kapteni Wang Yongfong alibeba notebook ya ASUS U5 hadi kwenye kilele. Katika mita 8,848 juu ya kiwango cha bahari, notebook za ASUS zilikuwa za kwanza ulimwenguni kufika juu ya kilele cha Mlima Everest.

    Hadi kwenye vizio vya mbali vya dunia

    Kwa mara nyingine notebook za ASUS zimethibitisha uwezo wake wa kukabili baridi kali sana ya Vizio vya Kaskazini na Kusini vya dunia.

    Mnamo Desemba 16, 2003, Shiang Wag na Jian Liu walianza safari yao ya kwenda kwenye kilele cha Mlima Vinson wenye futi 16,000, kilele cha juu zaidi katika bara la Antaktika, ambapo joto lilijulikana kuwa chini ya nyuzi -100˚F. Wapanda mlima hawa walibeba notebook ya ASUS S200N ili kuandika yale waliyoyaona. S200N ilikidhi mahitaji yao kikamilifu: ilikuwa nyepesi na imara, ilikuwa na uwezo mkubwa wa diski kuu na iliweza kumudu matatizo ya kukwea mlima.

    "Walifanya kazi bila tatizo kwenye mazingira magumu na hali mbaya ya hewa. Ilikuwa ni vizuri kuwa na notebook ambayo ingeweza kufanya kazi kwenye mazingira ambayo matatizo hayaepukiki,, " Wang alisema.