Kuhusu ASUS

  GreenASUS: Kuweka mazingira mawazoni

  Sisi katika ASUS tumejitolea kikamilifu kujenga mazingira endelevu siku zijazo. Tuna imani katika kujenga mazingira rafiki kuelekea kwenye kila eneo la biashara yetu. Hapa ndipo ambapo falsafa ya kijani ya ASUS hutokea — kutoka kwenye shughuli zetu za ndani hadi kwenye michakato yetu ya uzalishaji, kwenye bidhaa zetu za kijani pamoja na wafanyakazi wetu wenye ufahamu wa kimazingira — tunabakia kwenye shabaha ya kulinda dunia yetu.

  ASUS ilizalisha motherboard ya kwanza duniani isiyokuwa na madini ya risasi wala Halogen — pamoja na Kioo Onyeshi cha HD cha kwanza kisichokuwa na Halogen. Tulikuwa pia watengenezaji wa kwanza wa notebook kupokea EPD pamoja na hati za Eco za EU Flower na kuwa miongoni mwa wazalishaji 10 wa kwanza wa TEHAMA kupokea Japan Eco Mark.

  ASUS ilitambuliwa kwa Muundo wa Bidhaa Yake yenye Ufanisi wa Nishati katika Sherehe ya Tuzo ya ENERGY STAR ya 2011 — shukrani ziende kwa Teknolojia ya Super Hybrid pamoja na teknolojia za Green LCD.

  Hivi leo, teknolojia za kipekee za ASUS zinaendelea kuundwa na kuboreshwa kwa lengo kuu akilini la uhifadhi wa mazingira. Mbali na teknolojia hizi, hatua nyingine ambazo ni rafiki kimazingira hujumuisha utokomezaji wa vitu vyenye madhara toka kwenye mchakato wa uzalishaji pamoja na matumizi ya vifaa vya ufungashaji vinavyoweza kubadilishwa na kuundwa vitu vingine.

  GreenASUS ina vitu vifuatavyo:

  Muundo wa Kijani

  Bidhaa za miundo ambazo ni rahisi kutumika tena, na kuundwa upya, huboresha ufanisi wa nishati wa bidhaa, na husisitiza kuzingatia miongozo kuhusu vitu hatari.

  Uzalishaji wa Kijani

  Huweka mchakato wa uzalishaji wa kijani zaidi ambao hauna madini ya risasi wala halojeni.

  Ununuzi wa Kijani

  Inasimamia mfumo wa usimamizi wa ugavi wa kijani (SRM) na inasimamia database ya mtandaoni ya wauzaji wa kijani.

  Huduma za Kijani na Masoko

  Inasaidia programu za kuunda upya na kuhakikisha kuwa mashirika ya hisani yanafaidika na mipango hii.

  Mambo muhimu ya ASUS ya Kijani

  Kwenda zaidi ya kufuata sheria

  Mwongozo wa RoHS hauruhusu matumizi ya vitu 6 vya hatari lakini ASUS inazuia zaidi vitu 31 vya ziada kwa ajili ya usalama wa wateja wake, wafanyakazi na Dunia.

  Hati za IECQ HSPM kwa ajili ya HQ na maeneo ya viwanda

  ASUS imepata IECQ (IEC Quality Assessment System for Electronic Components) hati za HSPM (Hazardous Substance Process Management) kwa makao makuu yake na maeneo yake yote ya viwanda. IECQ hutoa kujulikana na uhakikisho wa kujitegemea kuwa vipengele vya kielektroniki, vifaa vinavyohusiana na taratibu vinazingatia viwango vinavyofaa, vipimo au nyaraka zingine.

  Inajulikana kama kampuni rafiki kwa mazingira

  ASUS imetambuliwa kama kampuni rafiki kwa mazingira katika Sekta ya Kompyuta na Vifaa vyake na Oekom research AG, taasisi ya kujitegemea ya utafiti iliyojikita kwenye tathmini ya wajibu wa kampuni.

  Matukio muhimu ya ASUS ya kijani

  2011

  • Ilipokea tuzo ya 2011 ya ENERGY STAR kwa Ubora katika Muundo wa Bidhaa yenye Ufanisi wa Nishati
  • Ilipokea "Tuzo ya Kijani ya TEHAMA" kwa ajili ya Kioo onyeshi cha VW247H-HF na U43SD Bamboo NB

  2010

  • Yakwanza kati ya watengenezaji 10 bora wa vifaa vya TEHAMA na Kompyuta kupata Japan Eco Mark
  • Iliwasilisha Motherboard ya kwanza duniani isiyokuwa na Halogen kabisa (P7P55D-E/HF)
  • Iliwasilisha modeli ya kwanza duniani isiyokuwa na Halogen kabisa ya LCD ya HD Kamili ya 1080p (VW247H-HF)
  • Notebook ya Had Bamboo ya U53Jc ilipokea PAS 2050/ ISO14067 Hati ya Carbon footprint
  • Notebook ya Had UL30A na Kioo Onyeshi cha VW247H-HF kiliwekwa kama Bidhaa Bora ya NB na Kioo onyeshi kwenye "2010 Greenpeace Electronics Survey"
  •Ilijiunga na Taiwan CSR rating kupitia "Great Vision Magazine" na kushinda CSR ya Ubora kwenye sekta ya TEHAMA
  •Ilijiunga na CSR Citizenship rating kupitia "CommonWealth Maganize" mnamo 2010 na ikaorodheshwa kwenye 10 bora

  2009

  Iliingia kwenye awamu ya uzalishaji usiokuwa na Halogen
  Ilipokea EPEAT Gold rating kwa ajili ya Eee PC™ Seashell netbook na vioo onyeshi tisa vya LCD
  Ilizalisha notebook ya kwanza duniani (N51V) kupata hati za Environmental Product Declaration (EPD) na carbon footprint (PAS 2050:2008)
  Ilipokea Hati ya EU Flower kwa ajili ya matoleo U ya notebook na EeeBox PC nettops

  2008

  Ilipokea hati ya EuP kwa ajili ya matoleo N ya notebook
  Ilipokea hati ya EU Flower kwa matoleo N na Bamboo ya notebook
  Ilipokea EPEAT Gold rating kwa matoleo N na Bamboo ya notebook
  Iliunda injini ya Super Hybrid kwa ajili ya notebook na injini ya EPU II-6 kwa ajili ya motherboard
  Ilizindua kioo onyeshi kinachotumia nishati kidogo cha VH192C/SC

  2007

  Iliunda ASUS AI Gear 2 kwa ajili ya motherboard
  Ilipokea hati ya IECQ HSPM kwa ajili ya HQ na maeneo ya uzalishaji
  Ilitambulisha Muundo wa Kijani kwenye mchakato wa uzalishaji "
  Ilianzisha mpango wa kutengeneza upya vifaa ndani ya Marekani

  2005

  Iliunda ASUS AI Gear kwa ajili ya motherboard

  2004

  Iliunda Power4Gear Plus kwa ajili ya notebook
  Ilizindua motherboard zisizokuwa na madini ya risasi

  2000

  Iliunda Power4Gear kwa ajili ya notebook

  "Sisi katika ASUS tunajivunia jitihada zetu za mazingira katika miaka iliyopita. Tutaendelea kujitoa ili kulinda kikamilifu rasilimali zetu za asili. Aidha, tutajitahidi kuzuia uchafuzi na tutaendelea katika ahadi yetu ya uzalishaji safi na uzalishaji wa kijani. "

  Jonney Shih, Mwenyekiti wa, ASUSTeK Computer Inc.