Kuhusu ASUS

  ASUS inachukua jina lake kutoka kwa Pegasus, farasi wenye mabawa katika elimu ya hadithi ya Kigiriki ambaye anaashiria hekima na ujuzi. ASUS inajumuisha nguvu, usafi, na roho inayojitokeza ya kiumbe hiki cha ajabu, na inaongezeka kwenye viwango vipya kwa kila bidhaa mpya inayoiunda.

  Sekta ya teknolojia ya habari mawasiliano ya Taiwan imeongezeka sana kwa miongo michache iliyopita na nchi sasa ni mshiriki mkubwa katika soko la kimataifa. ASUS kwa muda mrefu imekuwa mbele ya ukuaji huu na ingawa kampuni ilianza maisha kama mtengenezaji mdogo wa motherboard ikiwa na wafanyakazi wachache, sasa ni kampuni ya teknolojia inayoongoza nchini Taiwan na imeaajiri watu zaidi ya 11,000 kote duniani. Pia ASUS inatengeneza bidhaa karibu katika kila aina ya kategoria ya teknolojia ya habari mawasiliano, ikiwa ni pamoja na vipengele vya kompyuta (PC) na vifaa vyake vya pembeni, notebook, tableti, seva na simu za kisasa za mkononi (smartphones).

  Ubunifu ni msingi wa mafanikio ya ASUS. Kwa kuzindua PadFone kwa hadhira ya rapturous kwenye Computex 2011, mwaka huu Mwenyekiti wa ASUS Jonney Shih aliongeza kiwango cha mafanikio zaidi kwa tangazo la TAICHI na Transformer book-simu zenye matumizi zaidi ya moja.

  ASUS TAICHI ni Ultrabook yenye kuonyesha mara mbili ambayo inaruhusu itumike kama tableti wakati kifuniko kimefungwa, wakati Transformer Book ni tableti ambayo inaweza kufungwa kwenye kibodi kwa ajili ya mabadiliko ya papo hapo kuwa Ultrabook.

  Pamoja na Tableti ya 810 yenye Windows 8 na Tableti ya 600 yenye Windows RT, ASUS ina safu ya bidhaa ambazo zitazidi mawazo ya watumiaji wake wakati ulimwengu unapoingia kwenye zama mpya ya kompyuta mtandao.

  Mtazamo huu wa kimaono ni sababu ya kwa nini ASUS ni mshiriki mkuu katika kuleta uvumbuzi na muundo bora kwenye maisha ya watumiaji wake. Bidhaa za ASUS zilishinda tuzo za kimataifa 3,886 na zawadi mwaka 2011, na mapato ya kampuni yalikuwa zaidi ya $ 11.9 bilioni.