Kuhusu ASUS

  Kutengeneza Tena Upya PC kwa Ajili ya Baadaye Njema

  Mnamo Aprili 2008, ASUS iliungana na Intel na Tsann Kuen Enterprise kuzindua “Kutengeneza Tena Upya PC kwa Ajili ya Baadaye Njema” nchini Taiwan, mpango wa ushirikiano ambao unalenga kukusanya na kurejesha kompyuta za notebook za zamani, PC na vioo onyeshi vya LCD katika jitihada za kusaidia jamii zenye uhitaji pamoja na mazingira.

  Mpango wa “Kutengeneza Tena Upya PC kwa Ajili ya Baadaye Njema” unawahimiza watumiaji kurejesha vifaa vyao vilivyotumiwa kwenye vituo vya kuvikusanya, kama vile Vilabu vya Royal vya ASUS, maduka ya Tsann Kuen 3C na maduka ya DF Recycle. Vocha ya punguzo hutolewa kwa kila kompyuta ya desktopu, notebook au kioo onyeshi cha CRT / LCD bila kujali chapa ya kifaa kilicholetwa.

  Matokeo ya mpango huu, zaidi ya bidhaa 1,200 zilizotumika zilizopatikana kutoka kwenye mashirika, serikali na watu binafsi zilitengenezwa upya na hatimaye kutolewa kwa watumiaji wenye uhitaji. Wanufaika ni pamoja na shule 122 za awali na shule za sekondari, jumuiya tano za wazawa na kituo cha Seli Shina cha Tzu Chi.

  Vile vile, ASUS — tangu Septemba 2006—imekuwa ikifanya mpango wa urejeshaji wa bure wa kompyuta zake za notebook kutoka kwa wateja wake wa Marekani. ASUS ni kampuni ya kwanza ya Taiwan kutoa huduma kama hiyo nchini Marekani.

  Kwa ushirikiano na Microsoft ili Kupunguza
  Mgawanyiko wa Kidigitali

  ASUS imetoa kompyuta 500 za Eee PCs ™ zenye programu ya Windows kwa awamu ya nne ya mpango wa Microsoft Unlimited Potential (UP) kwa wanawake wa nchini Taiwan. Programu ya UP ya Wanawake hutoa mafunzo ya ujuzi wa TEHAMA kwa wanawake wote ambao wana mawasiliano uelewa mdogo wa teknolojia. Kwa kuonyesha jukumu ambalo TEHAMA inaweza kufanya kwenye maisha yao na kuwasaidia kujenga ujasiri wao, mpango huu unatarajiwa kupunguza mgawanyiko wa kidigitali ulioko kwenye jamii ya Taiwan.

  Kati ya Eee PCs ™ 500 zilizotolewa, 336 zilitolewa kwa vituo 15 vya teknolojia nchini Taiwan, na 44 zilitolewa kwenye kitengo jongevu cha UP ambacho kinatoa mafunzo katika maeneo ya vijijini ya kisiwa hicho, wakati 120 zilizobaki ziligawanywa kwa watu wakujitolea kwa ajili ya kufundishia. Tangu 2005, zaidi ya wanawake 50,000 wamefaidika kutokana na mpango huu. Lengo la ASUS ni kutoa mafunzo kwa wanawake zaidi ya 30,000 nchini Taiwan mwishoni mwa mwaka 2008.

  Kuwezesha Utoaji wa Elimu Ubora Duniani Kote

  ASUS hutoa msaada kwa taasisi za elimu na mashirika kwenye nchi kama vile Urusi, Jamhuri ya Czech, Uholanzi, na Ujerumani. Nchini Ujerumani, kwa mfano, ASUS inashiriki kwenye mipango kadhaa inayoendelea inayolenga kuhimiza matumizi ya TEHAMA katika elimu ya watoto. Hatua hizi zinajumuisha kudhamini Eee PCs ™ kwa shule moja kwa moja au kupitia washirika rasmi, kama vile N-21, taasisi rasmi ambayo hutoa vifaa vya kompyuta kwenye shule. Kwa msaada wa ASUS, shule zimepata uwezo wa kuingiza teknolojia za kisasa kama vile Web 2.0 kwenye njia zao za kufundishia, na hivyo kuimarisha ujifunzaji-binafsi kwa watoto kwa kuwaelimisha manufaa ya kuingia kwenye bahari kubwa ya ujuzi inayopatikana kwenye Mtandao wa Intaneti.