Kuhusu ASUS

    Mtengenezaji Nambari 1 wa Motherboard Ulimwenguni

    ASUS ni mtengenezaji namba moja wa motherboard ulimwenguni, ikitawala karibu sehemu ya soko ya 40% ya biashara ya motherboard. Zaidi ya motherboard milioni 420 zimeuzwa tangu 1989. Hivi leo, moja kati ya kila kompyuta tatu ina motherboard ya ASUS.

    Ilichaguliwa kuwa “Chapa Bora ya Motherboard” kwa miaka sita mfululizo

    ASUS ilichaguliwa kuwa “Chapa Bora ya Motherboard” ulimwenguni kwa miaka sita mfululizo na wasomaji wa Tom's Hardware Guide (THG), tovuti ya mapitio ya vifaa inayosomwa na kuheshimiwa sana. Katika kura hizi nyingi, ambazo kwa kawaida huhusisha makumi ya maelfu ya wapiga kura, ASUS imepata zaidi ya nusu ya kura.

    Tuzo Bora ya Chaguo la Wasomaji wa THG hutambua bidhaa za vifaa ambazo zinaonyesha usanifu wa ubora wa juu na makampuni ambayo yametoa huduma bora kwa watumiaji. Tuzo hizo zinachukuliwa kama ni alama ya usanifu bora wa bidhaa, ufanisi, ubora na thamani.

    Kiongozi asiye na Mshindani kwenye Ubunifu wa Motherboard

    ASUS imebahatika kuwa na moja kati ya timu bora za Utafiti na Maendeleo Duniani. Kila mara wanaendelea kusukuma mipaka ya uvumbuzi, na kuzalisha vipengele na teknolojia ambazo zimebadilisha tasnia ya motherboard kwa kufungua hazina zaidi, ustawi na ufanisi katika matumizi ya nishati. Baadhi ya hatua hizi muhimu katika maendeleo haya ni pamoja na:

    16 +2 Phase Power

    ASUS mapinduzi ya muundo wa 16-phase power hutumia kanuni halisi ya kutawala nguvu ya vifaa ili kuhakikisha ufanisi wa nguvu halisi—hadi 96% zaidi ya bidhaa za washindani. Mmotherboard za ASUS zenye kipengele hiki hutumia nishati kidogo na hufanya kazi kwa joto la chini, bila kuharibu kiwango cha ufanisi wake wa kipekee wa utendaji.. Kuongezeka huku kwa ufanisi kunaokoa pesa za mtumiaji, kupunguza joto ndani ya kompyuta (PC) na kurefusha maisha ya sehemu zake muhimu kama vile CPU na motherboard.

    Energy Processing Unit (EPU)

    EPU ya kipekee ya ASUS ni kipengele cha vifaa ambacho kinadhibiti vipengele sita vikuu: CPU, kadi ya VGA, hazina data, chipset, diski ngumu, na kipoozaji cha CPU/feni ya mfumo. Ikiwa na hazinadata iliyo na maelezo yote ya Intel CPU, EPU hufafanua kwa uwazi na kuchagua chaguo sahihi na inalinganisha mipangilio inayofaa ili kuhakikisha utawala bora wa nishati.

    Express Gate

    Express Gate ya kipekee ya ASUS inawezesha mfumo wa kompyuta kwenda mtandaoni ndani ya sekunde tano mara baada ya kuwaka. Kwa upatikanaji wa haraka wa Intaneti, watumiaji ambao daima wamefungwa kwenye muda watakuwa na uwezo wa kufurahia video za mtandaoni, kwa urahisi kutumia programu maarufu za Instant Messengers (IM) , kuangalia ripoti ya hali ya hewa au barua pepe kabla ya kuondoka nyumbani.

    Drive Xpert

    Drive Xpert ni suluhisho la vifaa la RAID ambalo ni bora kwa watumiaji ambao wanahitaji kulinda data kwenye diski yao kuu au kuboresha utendaji kazi wa diski kuu bila usumbufu wa kusakinisha viendeshi au kubadili mipangilio ya mfumo wa BIOS. Kwa kupitia Drive Xpert yenye kiolesura picha rafiki kwa mtumiaji na chelezo zenye nguvu, watumiaji wanaweza kupanga kwa urahisi chelezo za diski kuu, au hata kuongeza viwango vya kuhamisha data.

    TweakIt

    Ili kuwasaidia overclockers kujenga mashine yenye kasi sana kwa muda mfupi kadri iwezekanavyo, ASUS imeunda suluhisho la kibunifu la overclocking: TweakIt. TweakIt inawezesha overclockers kufanya mabadiliko ya wakati halisi kwenye mzunguko wa mifumo yao ya msingi, volti na vigezo vingine kwa kutumia udhibiti rahisi sana kwenye motherboard yenyewe—hata wakati programu za kipimo teule zinafanya kazi. Hakuna hatua ambayo programu inahusika; marekebisho yote yanafanyika kwenye msingi wa vifaa.

    Kwa Kuzingatia Kwanza-kuuza Bidhaa Inayojumuuisha Teknolojia ya Karibuni

    Kama kiongozi katika ubunifu wa motherboard, ASUS daima iko mbele kwenye maendeleo ya teknolojia. Kwa miaka mingi, imeongoza madai ya kuwa ya kwanza duniani. Ilikuwa mtengenezaji wa kwanza wa kuanzisha mamaboard zinazofanya kazi na Serial za ATA na AGP8X, P4 CPUs ya hadi 3GHz na zaidi, Teknolojia ya Hyper-Threading, Processor za Intel® Core ™ 2, na Windows Vista, hizi ni baadhi ya nyingine nyingi.

    Ikiwa inalenga mwenendo wa sekta hiyo na ushirikiano wa karibu na makampuni ya kibiashara ya TEHAMA yanayoongoza ulimwenguni, ASUS itaendelea kuwa ya kwanza kwenye soko kwa bidhaa bora za kisasa.